Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi
wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi
mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei,
2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza
kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).
2.0 WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA
Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa
mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za
kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na
Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za
mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na
kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe
kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni
kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu
kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza
kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi
anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.
Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya
kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa
mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango
cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha
ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu,
mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo
hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni
muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo,
kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa
wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014.
3.0 IDADI YA WANAFUNZI WALIOKWISHAOMBA MIKOPO KUFIKIA MEI 30, 2013
Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Na.
|
Waombaji wa mara ya kwanza waliokamilisha kujaza fomu
|
Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji
|
Wanafunzi wanaoendelea na masomo waliojaza fomu na kukamilisha
|
424
|
5320
|
60367
|
4.0 HITIMISHO
Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:
(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.
(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa
wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika
mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga
namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku
za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri
siku ya jumamosi.
(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment