Monday, June 10, 2013

GAKONDO GROUP- KIGALI RWANDA KUACHIA ALBUM MPYA.

Kikundi maarufu cha ngoma za kiutamaduni na asili nchini Rwanda - Kigali kinachoitwa Gakondo Group, ambacho ni moja kati ya vikundi maarufu kinachoongoza nchini humo wapo mbioni kutoa albamu yao ya kwanza kabisa kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.

Kiongozi wa kikundi hicho Intore Masamba, ameelezea kuwa hivi sasa albamu hiyo ipo katika matayarisho makubwa na tarehe rasmi ya uzinduzi wa albamu hiyo itatolewa muda wowote kuanzia sasa.

Aidha albamu hiyo inatarajiwa kusheheni nyimbo 12  zikiwemo Inanga, Icyembe, Ingoma na Umuduri, ambazo zote zimerekodiwa kwa kutumia vyombo vya asili akiweka wazi kuwa dhumuni la kutoa albamu hiyo ni kulinda na kuthamini utamaduni wa Rwanda kupitia muziki huku akiwahimiza vijana kutambua na kuipenda asili yao badala ya kupotoshwa na tamaduni za nje.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...