Friday, July 19, 2013

TFF YATANGAZA MAJINA YA VIONGOZI WA KAMATI MBALI MBALI.


Rais wa TFF Leodgar Chilla Tenga alitangaza  majina ya wajumbe wanaounda kamati za TFF jana. Walioteuliwa ni pamoja na Jaji Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto walioteuliwa kuziongoza kamati muhimu za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoundwa baada ya kufanyika mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho hilo mwishoni mwa wiki iliyopita,

Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati ya Rufaa na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...