Thursday, July 18, 2013

SHULE ZA UMMA ZAFUNGWA NCHINI KENYA.

Wanafunzi nchini Kenya wakiwa darasani.
Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za msingi za umma kufuatia huku walimu wa shule za umma za msingi na sekondari wakisitisha mgomo wao baada ya serikali kutangaza uamuzi huo.
Waziri wa elimu prof Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ameshutumu walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.
Zaidi ya walimu laki mbili na arobaini wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakidai nyongeza ya asili mia mia tano ya mishahara waliyoahidiwa na serikali mwaka wa 2007.
Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya usafiri, ya nyumba na matibabu. Serikali imesema kuwa wazazi wataarifiwa juu ya siku ya kufunguliwa tena shule.
Waziri huyo wa elimu amesema kuwa wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nane wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya miezi minne ijayo.

Source: BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...