Friday, March 1, 2013

MSAKO MKALI WA UCHIMBAJI WA MADINI KANDO MWA BWAWA LA MINDU.

Ndg.Christopha Evarist Bengu aliyekamatwa akichimba madini kando mwa Bwawa la Mindu.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) inaendelea na zoezi la kuhifadhi mazingira katika vyanzo vyake vya maji kwa wakazi wa Morogoro.Katika kuhakikisha hilo leo Maaskari wanaolinda Bwawa la Mindu wameweza kuwakimbiza watu zaidi ya kumi (10) waliokuwa wanachimba madini lakini wakafanikiwa kumkamata mchimbaji mmoja.

Ndg.Christopha Evarist Bengu akiwa chini ya ulinzi
Akiongea na Blogu hii Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita amesema mtuhumiwa huyo aitwaye Ndg.Christopha Evaristi Bengu anapelekwa Polisi kwa kuweza kupelekwa Mahakamani.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita.
Ikumbukwe kwamba wakazi wa Morogoro mpaka sasa wana uhaba mkubwa wa maji kutokana na ukame unaosababishwa na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wakazi wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...