Monday, July 1, 2013

WATANZANIA MILIONI 32 KUPATA MAJI IFIKAPO 2016.


Waziri wa Maji Prof.Jumanne Maghembe.
Serikali imesema hadi ifikapo mwaka 2016 zaidi ya Watanzania milioni 32 nchini sawa na asilimia 74 watapata huduma ya maji safi na salama.

Hayo yalisemwa  jana mjini Dodoma na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe kwenye hafla fupi ya kuwaaga wajumbe zamani wa Bodi ya 5 ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa) na kuikaribisha Bodi mpya ambayo ipo chini ya Mwenyekiti Balozi Job Lusinde.

Profesa Maghembe alisema kwa upande wa vijijini kwa sasa ni asilimia 57 ya watu ndiyo wanaopata  maji safi na salama.

Alisema miradi ambayo inatekelezwa hivi karibuni vijijini inaonekana miundombinu yake imechakaa na watu wanaopata huduma hiyo bila tatizo ni asilimia 40.

“Uwezo wa kufanya hivyo tunao…iwapo hatutafanya vitu kama tulivyokuwa tunafanya zamani…bomba linatoa maji hapo badala la kulifunga mara moja tunaliacha,” alisema Akizungumzia kwa Mji wa Dodoma, alisema watu wanaotakiwa kupata maji safi na salama ni asilimia 99.

Kwa upande wake Balozi Lusinde alisema jitihada za Wana-duwasa zimezaa matunda kutokana na kupungua kwa kiwango cha upotevu wa maji kutoka asilimia 34 na kufikia 32.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...