UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA
(TFF)
14/08/2013
1. Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia
wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF utafanyika tarehe
20/10/2013 jijini Dar es salaam. Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za
uongozi wa TFF wanataarifiwa kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF
zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe 20 Agosti 2013
katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya Fedha), kuanzia saa 03:00
asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00
Alasiri tarehe 20 Agosti 2013.
2. Nafasi
zinazotangazwa kugombewa ni:
(i)
Rais wa TFF.
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF.
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF, nafasi kumi na tatu (13).
3. Mtu
yeyote anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti
yafuatayo:
(i)
Awe Raia wa Tanzania.
(ii)
Awe na kiwango cha elimu
kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari.
(iii)
Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira
wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)
Asiwe na hatia yoyote ya kosa la
jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)
Awe na umri wa angalau miaka 25.
(vi)
Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira
wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa
Miguu katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza.
(vii)
Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye
uwezo wa kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi.
(viii) Mtu
anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa TFF lazima awe na
kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe na uwezo na
haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
4. Ada za Fomu
za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo:
(i)
Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano
(Tshs. 500,000/=).
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi
Laki Tatu (Tshs. 300,000/=).
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
5. Kwa wale
ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao
wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena
ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati
wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Na.
|
TAREHE
|
SHUGHULI
|
1.
|
14/08/2013
|
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kutangaza Uchaguzi wa TFF, nafasi za kugombea na sifa
za kugombea uongozi wa TFF.
|
2.
|
16/08/2013 – 20/08/2013
|
Kuchukua
Fomu za maombi ya uongozi wa TFF kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi
ya TFF (Katibu Mkuu wa TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi
hadi saa 10.00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF
ni Jumanne tarehe 20/08/2013 saa 10:00 Alasiri.
|
3.
|
21-23/08/2013
|
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kupitia fomu za waombaji uongozi wa TFF. Kutangaza
matokeo ya upitiaji fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina
ya waombaji uongozi wa TFF (23/08/2013).
|
4.
|
24-26/08/2013
|
Kutoa
fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni
tarehe 26/01/2013 saa 10:00 Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu
Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za
Uchaguzi.
|
5.
|
27/08/2013 – 29/08/2013
|
Wawekaji
Pingamizi na waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya
TFF kutoa utetezi wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi.
|
6.
|
30/08/2013 - 03/09/2013
|
Usaili na
kutangaza matokeo ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi
wagombea matokeo ya usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea.
|
7.
|
04 – 06/09/2013
|
Kamati ya
Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya
Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa
maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF.
|
8.
|
04 – 06/09/2013
|
Kutoa
fursa ya kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF
Elections Appeal Committee) kwa masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa
zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya Rufaa zitapokelewa na Katibu Mkuu
wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 06/09/2013 saa 10:00 Alasiri.
|
9.
|
07-13/09/2013
|
Kamati ya
Maadili ya TFF kupitia mashauri yote yanayohusu Maadili na kuyatolea
uamuzi.
|
10.
|
14- 16/09/2013
|
Kamati ya
Maadili ya TFF kutoa matokeo ya maamuzi ya mashauri ya Maadili kwa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF na wagombea.
|
11.
|
17- 19/09/2013
|
Kukata
Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa
ni tarehe 19/09/2013 saa 10:00 Alasiri.
|
12.
|
20- 24/09/2013
|
Kusikiliza
Rufaa zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF na kutolea
uamuzi.
|
13.
|
25-27 /09/2013
|
Kamati ya
Rufaa ya Maadili ya TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na
Wagombea matokeo ya Rufaa zilizosikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
|
14.
|
28/09/2013- 02/10/2013
|
Kamati ya
Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza Rufaa za Uchaguzi kwa masuala
yasiyo ya Maadili.
|
15.
|
03-04/10/2013
|
Kamati ya
Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya
rufaa wagombea waliokata rufaa (zisizohusu mashauri ya Maadili). Aidha
Kamati ya Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa hizo.
|
16.
|
05/10/2013
|
Kutoa
orodha ya wagombea wote waliopitishwa
|
17.
|
06/10/2013- 19/10/2013
|
Kipindi
cha Kampeni kwa wagombea wote.
|
18.
|
20/10/2013
|
Uchaguzi
wa Viongozi wa TFF.
|
7. Uchaguzi
wa TFF unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za
TFF.
Hamidu Mbwezeleni
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF
No comments:
Post a Comment