ALICHOKISEMA ZITTO KABWE LEO.
Kimsingi Serikali ilidanganya Bunge ili Bunge
lipitishe bajeti ya Wizara ya Ujenzi mwaka 2011/12. Mawaziri Magufuli na
aliyekuwa Naibu yake Mwakyembe na Waziri wa Nchi Lukuvi kwa nyakati
tofauti walidanganya Bunge ili kupitisha jumla ya shilingi 252 bilioni.
PAC imeamua mawaziri hawa Waende kamati ya maadili ya bunge ili
kujieleza na kuadhibiwa kwa uwongo wao.
Magufuli - 'tunaomba
fedha tshs 252 bilioni kwa ajili ya KUANZA kazi za ujenzi wa barabara' -
2011...
Mwakyembe - 'fedha hizi zitachangia
miradi ya wafadhili' 2011
Lukuvi - 'hizi ni fedha kwa ajili ya
counterpart fund' 2011
2013
CAG - 'hizi fedha za miradi
hewa na kasma kivuli'.
Magufuli - ' tulilipa madeni'
Katibu Mkuu 'tulilipa madeni'
PAC ' kwanini mlidaganya
Bunge'? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za
madeni? Kwanini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?
Uamuzi
CAG akague fedha zote za kasma hii hewa na
kuripoti fedha hizi zimekwenda kwa wakandarasi gani na kutoa taarifa
kwenye kamati mwezi oktoba.
Mawaziri wote waliodanganya
Bungeni watashtakiwa kamati ya maadili na kudanganya bunge kwa lengo la
kupitisha bajeti ya tshs 252 bilioni kufadhili miradi hewa.
Source:Zitto Social Media.
No comments:
Post a Comment