Monday, August 19, 2013

MTAZAMO WA ZITTO KABWE JUU YA RASIMU YA KATIBA.

Rasimu ya Katiba ibara ya 215 inasema vyanzo vya mapato ya Muungano, kikubwa, ni ushuru wa bidhaa. Wajumbe wa Tume wanasema walifanya hesabu sawa sawa na fedha hizo zitatosha kuendesha Muungano. Lazima aliyewafanyia hayo mahesabu ama aliwapotosha au hajui.
Mwaka 2012/13 Ushuru wa bidhaa (ndani na nje) uliingiza mapato ya tshs 1.5 trilioni tu. Fedha hii inatosha kuendesha Wizara ya Ulinzi peke yake!
Haitoshi hata kuhudumia Deni la Taifa (ambalo mkopaji ni Jamhuri ya Muungano). Huu muungano utaendeshwaje?
Rasimu inapaswa kufanyiwa kazi sana. Nahisi Tume ilikuwa na haraka na haikutafakari kwa kina baadhi ya masuala.
Mambo ya Muungano inabidi yaangaliwe upya kabisa ili kuboresha mfumo wa Serikali 3 unaopendekezwa ikiwemo kuzuia Washirika wa Muungano kuunda vikosi vyao vya kijeshi, Ulinzi na usalama. Suala la biashara ya kimataifa na hata suala la usimamizi wa maliasili (regulatory function).
Source:Zitto Social media.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...