Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Dorothy Gwajima akitoa ufafanuzi wa masuala ya afya kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) waliomtembelea ofisini kwake. |
Baadhi
ya wananchi wanaomeza dawa za kutibu kichocho na minyoo ya tumbo
kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
nchini (NTD), wanadai zinawasaidia kuongeza nguvu za kiume wakati wa
tendo la kujamiana.
Mratibu
wa mpango huo mkoa wa Singida Yuda Machumu, amesema hayo wakati
akiongea na waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya siku nne mjini
Singida ya uandishi sahihi wa taarifa zinazohusiana na masuala ya afya.
Amesema
kuwa baadhi ya wananchi hao wakishatumia dawa hizo hurudi tena kwa
wagawa dawa wakihitaji kupatiwa tena dawa, kwa madai kwamba zinawasaidia
sana kuwaongezea nguvu wakati wa kujamiana.
Machumu
amesema kuwa tatizo hilo haliwahusu wanaume pekee bali wanawake pia
ambao katika halmashauri ya wailaya ya Singida, baadhi yao hufika kwa
wagawa dawa kuomba dawa hizo, wakidai zinawasaidia sana kuongeza nguvu
ya mwili mara baada ya kumeza.
Akizungumzia
tatizo hilo, Machumu amesema siyo kweli kuwa dawa hizo zinaongeza nguvu
za kiume, hali hiyo hujitokeza baada ya kuwa dawa hizo zimeua vimelea
wa maradhi hayo mwilini ikiwemo wale wa minyoo na kichocho, hivyo mwili
kuwa na nguvu mpya.
Kwa
mujibu wa Machumu katika kipindi cha mwaka jana, mpango huo ulihudumia
zaidi ya watu 850,000 sawa na asilimia 71 ya lengo la kuhudumia watu
1,205,159 kwa mkoa wa Singida.
CHANZO MO BLOG
No comments:
Post a Comment