Tuesday, August 27, 2013

TAARIFA KUHUSU KUFUKUZWA KWA MBUNGE WA KIEMBESAMAKI NA KUTEULIWA KWA MAKATIBU WAKUU WAPYA CCM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
1.   Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.   Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.   Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013


MAKATIBU WA CCM WA WILAYA WALIOTEULIWA NA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA TAREHE 23/08/2013.



1.           Ndugu Ashura Amanzi
2.           Ndugu Rukia Saidi Mkindu
3.           Ndugu Elias J. Mpanda
4.           Ndugu Jonathan M. Mabihya
5.           Ndugu Mulla Othman Zuberi
6.           Ndugu Jumanne Kapinga
7.           Ndugu Ali Haji Makame
8.           Ndugu Jacob G. Makune
9.           Ndugu Juma A. Mpeli
10.        Ndugu Hawa Nanganjau
11.        Ndugu Abdulrahman Shake
12.        Ndugu Subira Mohamed Ameir
13.        Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
14.        Ndugu Juma Bakari Nachembe
15.        Ndugu Josephat Ndulango
16.        Ndugu Rajab Uhonde
17.        Ndugu Abeid Maila
18.        Ndugu Mohamed Lawa
19.        Ndugu Mariam Sangito Kaaya
20.        Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
21.        Ndugu Julius Peter
22.        Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
23.        Ndugu Mathias Nyombi
24.        Ndugu Mohamed Hassan Moyo

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...