CHADEMA jana kimeanza rasmi kuendesha mabaraza ya Katiba na taarifa hii ndiyo iliyotolewa:-
"Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza
ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni
yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Mikutano ya
hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa
na
timu mbili
za viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt.
Willibroad
Slaa.
Mikutano
hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa
umma,
kupitia
vyombo vya habari (mainstream & social media).
2. Kutuma
ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba
Mpya
kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.
3. Email; chademamaoni@gmail.com & chademamaoni@chadema.or.tz
4. Mitandao ya
kijamii, mf; Jamii Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m
mabadiliko,
wanabidii
n.k, utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa
ni
pamoja na
kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni
yao kwa
njia hii.
Tumaini Makene
CHADEMA Senior
Information(Press) Officer
0752 691569/
0688 595831"
Source:CHADEMA Social Media.
No comments:
Post a Comment