Tuesday, February 19, 2013

NUSU YA WATAHINIWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE WAPATA SIFURI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012

1.0  UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1  Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176. Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani. 

2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.

3.1 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa
 (a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67.  Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012  ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50.  Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro,  ugonjwa na vifo.
(c)  Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084  wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23  hawakufanya mtihani.
4.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a) Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.
(b) Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361. 
5.0 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:

Idadi ya Wavulana      
Idadi ya  Wasichana
Jumla
I
1,073
568
1,641
II
4,456
1,997
6,453
III
10,813
4,613
15,426
I-III
16,342
7,178
23,520
IV
64,344
38,983
103,327
0
120,664
120,239
240,903
6.0 SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5.  Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
ST. FRANCIS GIRLS
90
MBEYA
2
MARIAN BOYS S.S
75
PWANI
3
FEZA BOYS S.S
69
DAR ES SALAAM
4
MARIAN GIRLS S.S
88
PWANI
5
ROSMINI  S S
78
TANGA
6
CANOSSA S.S
66
DAR ES SALAAM
7
JUDE MOSHONO S S
51
ARUSHA
8
ST. MARY’S  MAZINDE JUU
83
TANGA
9
ANWARITE GIRLS S S
49
KILIMANJARO
10
KIFUNGILO  GIRLS S S
86
TANGA
11
FEZA GIRLS
49
DAR ES SALAAM
12
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
124
KILIMANJARO
13
DON BOSCO SEMINARY SS
43
IRINGA
14
ST.JOSEPH MILLENIUM
133
DAR ES SALAAM
15
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
64
KIGOMA
16
ST.JAMES SEMINARY SS
44
KILIMANJARO
17
MZUMBE SS
104
MOROGORO
18
KIBAHA SS
108
PWANI
19
NYEGEZI SEMINARY SS
68
MWANZA
20
TENGERU BOYS SS
76
ARUSHA

7.0 SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
MIBUYUNI S.S
40
 LINDI
2
NDAME  S.S
41
UNGUJA
3
MAMNDIMKONGO S.S
63
PWANI
4
CHITEKETE S.S
57
MTWARA
5
MAENDELEO S.S
103
DAR ES SALAAM
6
KWAMNDOLWA S.S
89
TANGA
7
UNGULU S.S
62
MOROGORO
8
KIKALE S.S
60
PWANI
9
NKUMBA S.S
152
TANGA
10
TONGONI S.S
56
TANGA

8.0 TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA   KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 
8.1 Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.  Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i) Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii) Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2 Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule.  Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii) Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.
(iii) Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.
(iv) Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v) Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.
9.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a) Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
(b) Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
10.0 MATOKEO YA MITIHANI  YALIYOFUTWA
10.1  Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17. Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:
S/N
AINA YA UDANGANYIFU
IDADI YA WATAHINIWA
(i)        
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
04
(ii)       
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
170
(iii)      
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
590
(iv)      
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
04
(v)       
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
06
(vi)      
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
15
JUMLA
789

10.2 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao

(i) Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“Written responses to any examination question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo  yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:  
“A candidate found to have committed an examination offence shall – (a) have his examination results nullified”
(ii)Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti) kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania  kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0 KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012
(a) Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012  yanapatikana katika tovuti zifuatazo: 
     ·   www.matokeo.necta.go.tz,
    ·  www.necta.go.tz,     
    ·  www.udsm.edu.ac.tz, au
    ·  http://www.moe.go.tz
(b) Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya  ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
                                  (Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt.  Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

18 Februari 2013

Monday, February 11, 2013

BREAKING NEWS: MAPIGANO YA KIDINI YAPOTEZA MAISHA YA RAIA BUSELESELE GEITA

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa kumezuka mapigano kati ya Waislam na Wakristu huko Geita .Inadaiwa katika machafuko hayo,mtu mmoja amepoteza maisha kufuatia sakata la uchinjaji nyama ambapo inasemekana wachungaji wa kanisa la AIC wamewatangazia waumini wake kutokula nyama inayochinjwa na Waislam na kwamba leo wakristo wa eneo la Buselesele wamefungua Mabucha yao na kuanza kuuza nyama. Tutaendelea kuwapasha habari zaidi kadri tutakavyokuwa tunazipata habari.

Tuesday, February 5, 2013

KITALE AFUNGA NDOA NA KUUAGA UKAPELA.

Kitale akiwa na mkewe Bi Fatuma
 Hatimaye msanii wa filamu za komedi ameamua kuuaga ukapela na kuoa baada ya hiyo jana kufunga pingu za maisha na mke wake Bi Fatuma Salumu.
Kitale akiwa anafungishwa nikhai
 Ndoa hiyo ilifungiwa maeneo ya Mwananayamala jijini Dar es salaam mnamo saa nane hivi mchana.Kama kazi yake inavyohakisi,sherehe za ufungaji wa ndoa hiyo ziliudhuriwa na watu wengi ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa.


Monday, February 4, 2013

BREAKING NEWS: MOTO WAIBUKA NA KUUNGUZA VITU STENDI YA MWENGE

Moto uliozuka katika maduka ya eneo la Mwenge kituo cha mabasi umedhibitiwa na vikosi vya zimamoto na sasa hali ni shwari ingawa shughuli nyingi za kibiashara bado zimesimama wahusika wakihofia usalama wa mali zao.

Friday, February 1, 2013

BREAKING NEWS: MVUA ZALETA MAAFA MJINI MOROGORO

Barabara Morogoro ikiwa imejaa maji

Mvua zinazoendelea kunyesha mjini Morogoro zinazidi kuleta maafa baada mvua zilizonyesh usiku wa leo zimewaathiri wakazi wa hapa baada ya nyumba kujaa maji na baadhi ya barabara kufungwa kutokana na kujaa maji.
Maji yakiwa yamejaa barabarani eneo la Mtawala karibu na uwanja wa Shujaa


Magari yakiwa yanajiuliza namna ya kupita katika barabara Uwanja wa Shujaa.

Tatizo hili limeweza kuzikumba na baadhi ya Ofisi za Serikali ambapo katika ofisi za MORUWASA na Ofisi za Bonde la Wami/Ruvu maji yalijaa getini kiasi cha wafanyakazi wenye magari kushindwa kupita na kusubiri maji yapungue.

Geti la ofisi za MORUWASA na Bonde la Wami/Ruvu likiwa limejaa maji.


Thursday, January 31, 2013

HABARI ZILIZOVUNJIKAVUNJIKA:JAHAZI SUNRISE YAZAMA NUNGWI ZNZ

Jahazi SUNRISE ambayo ilikuwa ikitokea Mkoani Tanga kulekea visiwani Zanzibar ikiwa na abiria 32 imezama eneo la Nungwi huku jitihada za kuwaokoa abiria hao zikiendelea kufanywa na maofisa wa uokoaji mpaka sasa.
Kwa habari zaidi fuatilia hapa hapa.

KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOIVAA CAMEROON CHATAJWA,MAFTAH NA TEGETE WATOSWA.


Tegete kushoto akiwa na Kiiza

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI NA MAASKARI WENZAKE WAMCHEFUA HAKIMU.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi akiwa katika viwanja vya Mahakama

Askari waliomleta mahakamani mtuhumiwa askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)  wa mauwaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi,   wamemtibua Hakimu aliyeagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani hapo kwa kudharau mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa mnyeti wetu kutoka mahakamani hapo,tukio  hilo lilitokea leo  majira ya saa 5.35 asubuhi mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo. Askari  watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa  kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .

Mahakama ikiwa  bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi  wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani  huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza  kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.

Wakati hakimu  huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku  hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria  wa Mahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha  na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa  bila utaratibu wa mahakama hebu  mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona  wanafanya fujo mahakamani  hao.
Pamoja na jitihada za mwanasheria wa  serikali Adolf Maganda kuwaita  kwa  sauti,  askari hao  kuwataka  kumrudisha  ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo  bali  walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda naye mahabusu. 

Baada ya dakika kama 5 hivi, ndipo mwanasheria  huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambaye hata  hivyo hakwenda kusimama  kizimbani na badala  yake alikwenda upande wa  kushoto wa mahakama ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama  kuanza na kuketi katika  kiti huku akiwa bado amevaa miwani na kofia  yake.

Kutokana na  tukio  hilo, Hakimu  huyo alilazimika  kuwahoji askari hao  watatu kwa vurugu  hizo  walizozifanya kwa kuwauliza swali moja  pekee , ikiwa wanaona walichofanya ni  sahihi, ambapo askari hao waliosema, “samahani mheshimiwa”.

Mwendesha mashtaka  wa Jamhuri, Adolf Maganda aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena  kwa kesi hiyo ambayo awali ilikuwa imetajwa Januari 27, 2013 lakini mtuhumiwa alishindwa kufika Mahakamani kutokana na ugonjwa. Mahakama  hiyo  imeahirisha  kesi hiyo  hadi  Februari 14 mwaka huu.

Jinsi marehemu Mwangosi alivyokuwa akikabiliwa na maaskari kabla ya umauti kumkuta.
Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa  bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Ten  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  zilipozuka vurugu kati ya  Askari Polisi na wafuasi wa  CHADEMA.

Wednesday, January 30, 2013

WATUMISHI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAPATA AJALI

Gari la Wizara lililopinduka

Watumishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wapata ajali kilometa ishirini kabla ya kufika mkoa wa Dodoma wilaya ya Bahi,ajali hiyo ilisababishwa na cheni ambayo ilitumika kuwavuta maafisa wengine waliokwama wakiwa safarini kuelekea mkoani Mara (Musoma) kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya MTUHA,hali za watumishi (Enock Mhehe,Shoo,Mtimbika na Muhasibu kutokea Singida) zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu Hospitali ya mkoa Dodoma na kurushusiwa kuendelea na safari.

Magari yaliyopata ajali

MVUA ZILIZONYESHA JANA MOROGORO


Bwawa la Mindu

Jana kulinyesha mvua kubwa sana Mjini Morogoro kiasi cha kuwasababishia madhara baadhi ya wakazi wa Manispaa wanaoishi mabondeni ikiwa ni pamoja na kusombwa kwa baadhi ya nyumba.
Mkazi wa Morogoro akifurahi baada ya mvua kunyesha hiyo jana
Lakini pamoja na kunyesha kwa mvua hizo hali ya maji katika  bwawa la Mindu haikubadilika sana maana mpaka kufika leo saa 9.30 mchana maji yalikuwa yameongezeka kwa kiasi cha sentimeta sita (sm 6),lakini kiasi cha maji yanayoingia bwawani kinaweza kuwa kimebadilika na kuongezeka kufika kesho asubuhi maana mito inaendelea kuingiza maji bwawani.

TAIFA STARS KUKIPIGA NA CAMEROON

Kikosi cha Taifa stars

Timu ya taifa mpira wa miguu ya Tanzania Taifa stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Cameroon mchezo utakaopigwa Februari 06,2013 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 11 kamili jioni.
Kikosi cha Cameroon kinatarajiwa kuwasili hapa nchini tarehe 03 Februari,2013 kwaajiri ya mtanange huo.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo upo katika calenda ya FIFA,hivyo matokeo ya mchezo huo yanatumika kutuweka kwenye nafasi za viwango vya FIFA.

UKAME MKALI WAIKUMBA MOROGORO

Bwawa la Mindu likiwa limekauka kwa ukame

Hali ya mji wa Morogoro inazidi kuwa mbaya baada ya kutonyesha mvua kwa muda mrefu.Ukame huu umepelekea maji katika bwawa la maji la Mindu kukauka na kupungua kina cha maji kwa meta 2 (2m)
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mjisafi na Usafi wa mazingira Morogoro wamefanya ziara ya kutembelea vyanzo vya maji na kujionea upungufu wa maji .
Wajumbe wa Balaza la Wakurugenzi wa MORUWASA pamoja na watendaji wakiwa wanaangalia jinsi bwawa lilivyokauka.

Katika kujumuisha ziara hiyo,Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa amewasihi wananchi wote pamoja na wanasiasa kushirikiana katika suala zima la utunzaji wa mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita amesema suala hili la uharibifu wa Mazingira linasababisha "mgao wa maji ndani ya mgao" kutokana na upungufu huo wa maji.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita







Monday, January 28, 2013

LULU ARUDISHWA RUMANDE


Lulu akiwa na mwigizaji mwenzake Ray kabla ya kwenda mahabusu.

Katika hali isiyo ya kwawaida mwigizaji Elizabert Michael a.k.a Lulu amerudishwa rumande baada ya taratibu za dhamana kutokamilika. 
Lulu akipanda gari kurudishwa rumande
Lulu akitoka mahakamani

Kwa mujibu wa mhabarishaji aliyekuwa mahakamani hapo amesema Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa Mahakama ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo,hivyo dhamana yake inaweza kuwezekana keho.
Awali,Mahakama Kuu ya Tanzania iliweka wazi masharti ya dhamana ya msanii 
  huyo ambayo ilikuwa ni pamoja na:
  • Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
  • Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
  • Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
  • Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

HABARI ZILIZOVUNJIKA:LULU APEWA DHAMANA


Habari zilizopatikana hivi punde kutoka mahakamani zinasema kuwa Lulu amepewa dhamana na Mahakama kuu ya Tanzania baada ya mawakili wanaomtetea Lulu kuwasilisha ombi la dhamana mahakamani hapo.
Mawakili hao ambao ni Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliiomba mahakama hiyo itoe dhamana haraka kwakuwa mteja wao amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Ikumbukwe kuwa Elizabeth Michael anakabiliwa na kosa la kumuua mwigizaji mwenzake Kanumba bila kukusudia tukio lililotokea mnamo 07/04/2012


WIZARA YA AFYA NA AFYA YA JAMII. 
Wizara ya afya na ustawi wa jamii katika kuhakikisha kuwa inaboresha afya ndani ya jamii, imetangaza nafasi za mafunzo ya idara ya afya katika vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo. Nawaomba watanzania wenzangu tumia nafasi hii kuomba nafasi hizo.
Maelekezo yote kuhusiana na nafasi hizo yapo hapa chini kwenye tangazo kao.

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

         MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2013/14




Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara kwa mwaka wa masomo 2013/2014.



1.      Kozi zinazotangazwa ni:  



A.    Ngazi ya Stashahada:

(i)             Afisa Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)

(ii)           Fiziotherapia (Physiotherapy)

(iii)          Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)

(iv)          Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)

(v)           Optometria (Optometry)

(vi)          Tabibu (Clinical Officer)

(vii)        Tabibu Meno (Dental Therapist)

(viii)       Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)



B.    Ngazi ya Cheti



(i)             Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)

(ii)           Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)

(iii)          Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)

(iv)          Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)



C.    Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa (Distance Learning) kwa wale waliohitimu mafunzo ya Tabibu Msaidizi mwaka 2009.



2.     Muda wa Mafunzo:

(i)             Miaka mitatu kwa kozi za Stashahada

(ii)           Miaka miwili kwa kozi za Ngazi ya cheti

 


3.     Sifa za Muombaji:

Waombaji watarajali (Pre-service):

(i)             Awe raia wa Tanzania

(ii)           Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea

(iii)          Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  katika  masomo ya Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada . Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.

(iv)          Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.

(v)           Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua ‘E’,  kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha  mtihani.

(vi)          Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.





Waombaji wa Mafunzo ya Masafa (Distance learning:

  1. Wanaotakiwa kujiunga na Bridging course kabla ya kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya waganga wasaidizi vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.

  1. Tabibu wasaidizi (NTA 5) Wanaotakiwa kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne.

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Tabibu wasaidizi (NTA 5) mwaka 2009.

4.     Utaratibu wa kutuma maombi:

(i)    Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, Waganga Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara.

(ii)  Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, iwasilishwe pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).

(iii)Malipo  yaingizwe kwenye akaunti ,Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.

(iv)Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti halisi ya malipo ya Benki,  inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.

(v)  Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay  in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.

(vi)Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.

(vii)      Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa Katibu Mkuu,  wizara ya afya na ustawi wa jamii,kupitia anwani za wakuu wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.

(viii)    Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

a)      Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro.

b)     Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma

c)      Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.

d)     Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha CEDHA, S.L.P.1162, Arusha..

e)      Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.

f)       Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.

g)     Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe, S.L.P. 595, Dodoma.

h)     Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza.

i)      Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam.



5.     Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:

a)     Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara na mbao za matangazo Wizarani.  

b)     Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.



6.     Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2013.

7.     Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2013.



Imetolewa na:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

Dar es Salaam

Monday, January 21, 2013

UKUTA WA KITUO CHA MABASI UBUNGO WAANGUKIA MAGARI ZAIDI YA 24.
Muonekano wa namna ukuta ulivyoangukia magari
Katika hali ya kushangaza,magari zaidi ya 24 yameangukiwa na ukuta wa stendi ya mabasi Ubungo wakati mkandarasi akijaribu kubomoa ukuta huo kwa matengenezo.
Gari aina na suzuki likiwa nyang'anyang'a

Chanzo cha habari hii kinasema kuwa inasemekana kuna na majeruhi waliotokana na ajari hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Dar wakiwa wanashangaa ajari ilivyotokea.

Gari ndogo ikiwa hoi bini taabani.
Swali langu hapa ni "nani atakayewajibika na fidia?"


Thursday, January 17, 2013

HUU NI UZEMBE KAZINI USIO VUMILIKA.
Hiki ni kituo cha Afya cha Saba saba katika Manispaa ya Morogoro ambacho ni mojawapo ya ofisi za Serikali.Tarehe 13/11/2012 nilifika katika kituo hiki na kukuta BENDERA YA TAIFA ikiwa inapepea mida ya saa 1 usiku,nikasema labda yule mlinzi mwenye wajibu wa kuishusha anadharula.Lakini kitu cha kushangaza jana  tarehe 16/01/2013 usiku minamo saa 1 usiku pia bendera hiyo imekutwa bado inapepea wakati najua fika kuwa bendera inatakiwa kushushwa saa 12 jioni.

Nimekaa pale mpaka bendera hiyo imekuja kushushwa saa 1.28 usiku.


SWALI langu,ni je,taratibu za kushushwa kwa bendera zimebadilika au ni uzembe tuu wa watu wasiojali kazi zao.

Wednesday, January 16, 2013

OKWI HUYOOOOOOO TUNISIA


Picha ya Okwi akiwa anamiliki mpira.
  Emmanuel Okwi 
Hi guys thanks to God the deal is done.. Am officially a player of Etoile Sportive Du Sahel, it's really a new challenge and a big step for me in my carrier.. Let me take this chance to thank all Simba fans and officials for the support u gave me.. U were really special to me, god bless u all.. Alluta continua..
Hayo ni maneno yake Okwi aliyoyaandika katika ukurasa wake wa Facebook. 
Na kwa upande wa Simba sport club,kutokana na taarifa walizozisambaza kwa wapenzi wa timu hiyo kwa njia ya ujumbe mfupi leo hasubuhi ni kama ifuatavyo:  
"Hatimaye uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumuuza mshambuliaji wake Mganda Emmanueli Okwi kwa klabu ya Eoile du sahel ya Tunisia kwa ada ya dola laki 3" 
Namtakia kila la kheri huko aendako.

Tuesday, January 8, 2013

UDHAIFU WA WAKANDARASI WAZAWA KATIKA KAZI ZA UJENZI.
Barabara ya IPO IPO - KIHONDA MAGOROFANI

Umekuwa ni wimbo kuwa kazi nyingi za ujenzi wanapewa wakandarasi kutoka nchi za nje wakati wakandarasi wazawa wakinyimwa kazi.Malalamiko haya yanasikika kila mahali lakini je,sisi wazawa kazi zetu zinaridhisha???.
 
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina mkakati mzuri wa kuboresha barabara zake ili ziweze kupitika kirahisi ili kurahisisha  mawasiliano katika maeneo mbali mbali.Miongoni mwa barabara hizo ni ile ya IPOIPO - KIHONDA MAGOROFANI ambayo ilijengwa kwa kiwango cha lami.Ili kusikiliza kilio cha wakandarasi wazawa kuwa hawapewi kazi Manispaa ikampa kazi mkandarasi aitwaye:MAGINGA BUSINESS HOLDINGS CO Ltd,S.L.P. 1523,DODOMA.





Lakini kazi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa MHANDISI WA MANISPAA YA MOROGORO,kitu cha kushangaza nikwamba tangu kazi hii ikamilike haina miezi hata mitatu (3) lakini kwa mvua kidogo zilizonyesha tarehe 05/01/2013 zimebomoa barabara hii vibaya sana kiasi cha zile 'slabs' kuondoshwa na mvua pembezoni mwa barabara.

Swali langu ni je,barabara hii itadumu kweli?
Watanzania tuacheni kulalamika tu,tuwajibike na tuwe makini na kazi tunazofanya ili tuweze kuuza soko letu kitaifa na kimataifa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...