Takribani watu 15 wamejeruhiwa katika milipuko ya
maguruneti nchini Kenya Jumapili usiku. Mashambulizi hayo yalifanywa
mjini Mombasa mtaa wa Likoni na Nairobi katika mtaa wa Eastleigh yote
chini ya kipindi cha masaa mawili.
Shambulizi la mjini Mombasa, lilifanyika katika
kanisa moja saa moja usiku Jumapili na kuwajeruhi watu 12 wakati
shambulizi la Niarobi lilitokea katika hoteli moja huku watu watatu
wakijeruhiwa.Waathiriwa mjini Nairobi walikimbizwa hospitalini kwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta kwa matibabu zaidi.
Maafisa wakuu mjini Mombasa walielezea kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokana na shambulizi hilo lakini kulikuwa na ripoti kuwa baadhi ya waathiriwa walilazwa katika hospitali kuu mjini Mombasa wakiwa hali mahututi.
Polisi walisema kuwa watu sita akiwemo mwanfunzi wa darasa la nne pamoja na mhubiri walijeruhiwa katika kile kilichosemekana kuwa shambulizi la guruneti katika kanisa la Earthquake Miracle Ministries.
Waathiriwa zaidi walijeruhiwa katika msongamano wa watu waliokuwa wanakimbilia usalama wao baada ya kuzuka kwa moto kufuatia gurunti hilo.
Matukio hayo ya usiku wa kuamkia leo, yanazua wasiwasi kuhusu kuibuka tena kwa mashambulizi ya kigaidi katika miji hiyo miwili baada ya miezi kadhaa ya kutokuwepo mashambulizi.
Duru zinasema kuwa shambulizi la Nairobi lilitokana na guruneti lililorushwa kutoka kwa gari iliyokuwa inakwenda kwa kasi, wakati shambulizi la mjini Mombasa lilitokea wakati mtu aliyekuwa anaendesha pikipiki aliporushia guruneti kikundi cha watu.
Duru zinasema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mashambulizi hayo.
Kufikia Jumapili, usiku, wataalamu walikuwa bado wanakusanya ushahidi mjini Mombasa kubaini nia ya mlipuko uliotokea na ikiwa lilikuwa shambulizi la guruneti au kifaa kilichotengezwa mfano wa bomu.
Mashambulizi kama haya yamekuwa yakishuhudiwa tangu jeshi la Kenya kujiunga na majeshi ya AU katia harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram.
Source:BBC
No comments:
Post a Comment