Maduka yamesalia kufungwa mjini Kampala Ugana kwa siku ya tatu leo
huku wafnyabiashara wakigoma kuhusiana na mpango wa serikali kusisitiza
viwango vya biadhaa zinazoingizwa nchini humo kuwa za juu.
Chama cha wafanyabiashara hao
kinasema kinapinga gharama wanayotozwa ikiwa bidhaa wanazoingiza nchini
humo sio za viwango vya juu. Malipo hayo ni kodi iliyoanza kutozwa na
serikali hivi karibuni ambayo inagharamia kuchunguzwa kwa bidhaa
zinazoingizwa nchini humo
Wanatak serikali ikome kuwatoza ushuru huo kwani wafnyabiashara tayari wanatozwa kodi ya juu.
Duru zinasema kuwa vuguvugu la upinzani
linatarajiwa kujiunga na maandamano hayo, na kuwa polisi wamedhibiti
hali ya usalama mjini Kampala.
Mwandishi wa BBC mjini humo Catherine Byaruhanga
anasema kuwa polisi huenda wakavunja maandamano hayo kwa kuhofia otovu
wa usalama.
Waziri wa biashara, Amelia Kyambadde, ameelezea
wazi kuwa Uganda inashinikizwa na wanachama wa jumuiya ya Afrika
Mashariki kuwa iweze kutekeleza vikwazo vya kuhakikisha kuwa bidhaa
zinzoingizwa nchini humo ziwe za hali ya juu.
Kodi hiyo inalenga kuondoa uwezekano wa
wafanyabiashara kuingiza biadhaa ghushi nchi humo swala ambalo Uganda
inatuhumiwa kutokuwa maakini nalo katika kulitokomeza.
Wafanyabiashara wanapaswa kuingiza nchini humo
bidhaa za hali ya juu kutoka kwa watengezaji wanaojulikana na ambao wako
kwenye orodha inayojulikana kwa mataifa ya Afrika Mashariki, ingawa
wanasema kuwa gharama inayopaswa kulipwa kwa hilo kufanyika ni ya juu
zaidi.
Source:BBC
No comments:
Post a Comment