MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) Zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.
“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"
Aidha
Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza
kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo
itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa Zanzibar na Tanganyika kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
“Vijana
tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa,
taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na
usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai
nchi haitatawalika,” amesema
Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.
“Chama
pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo
mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji
kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo
ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa
Kwa
upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu
wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto
wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo
kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu
wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.
“Mikopo
ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima
tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo
kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni
tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.
Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana |
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa |
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro |
Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya |
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM |
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro. |
No comments:
Post a Comment