Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya
kinywaji chake cha Kilimanjaro, inaendelea na ziara ya tamasha kubwa la
muziki la ‘Kili Music Tour 2013’ ambapo wikiendi hii ya Jumamosi ya
tarehe 29 mwezi Juni, litafanyika Mjini Tanga kwenye kiwanja cha
Mkwakwani likijumuisha wasanii wakali wanane ambao ni Ally Kiba, Snura
Mushi, Professor J, Mwana FA, Recho, Mzee Yusuph, Roma na Kala Jeremiah.
Ziara ya Kili Music Tour ilianzia Dodoma wiki iliyopita na kuacha kumbukumbu isiyofutika kwa wakazi wa Dodoma na viunga vyake, ambao walipata burudani kutoka kwa wasanii nyota kama vile Ben Pol, Roma, Ally Kiba, Linex, Professa Jay, Ommy Dimpoz, Lady Jay Dee pamoja na Mkali Kala Jeremiah.
Kili Tour kwa mwaka huu inakujia ikiwa na kauli mbiu ya “Kikwetu kwetu” kwani burudani itayokuwa ikitolewa ni kutoka kwa wasanii wa nyumbani, wakikupa ladha za ala za muziki wa nyumbani na katika viwanja vya nyumbani.
Kama kawaida, mambo yataanza saa 10 jioni, jumamosi hii pale Mkwakwani na unakabidhi shilingi elfu mbili na mia tano mlangoni, ambapo utapata bia moja bureee, unaingia unapata burudani kutoka kwa wasanii bora kabisa Tanzania, Kili Music Tour 2013, Kikwetu Kwetu zaidi.

No comments:
Post a Comment