Chama cha kitaifa cha walimu nchini Kenya,
kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia leo baada ya serikali kukosa
kuwalipa marupurupu yao.Huu ni mgomo wa saba wa walimu tangu mwaka 2007.
Mwnyekiti wa kitaifa wa chama hicho,Wilson Sossion alituhumu serikali kwa kucheza siasa na maswala yanayowahusu walimu kwani wanafahamau masaibu ya walimu na mkataba wa mwaka 1997 uliotoa ahadi ya marupurupu hayo kwa walimu.
Kulingana na makubaliano hayo, serikali inapaswa kuwalipa walimu marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu , kuwlaipia nyumba , matibabu na pesa za usafiri.
"tumedurusu mienendo ya serikali na kugundua kuwa wantumia mtindo wa kugawanya watu. Hilo halitafanya halitafaulu,'' alisema bwana Sossion
"Tumetangza kuwa mgomo wa waalimu unaanza rasmi leo, '' aliongeza bwana Sossion
Sossion pia alisema kuwa tume ya kushughulikia maswala ya walimu, haina mamlaka ya kuwaamuru walimu kutogoma au vinginevyo kwani hilo ni jukumu la Knut.
Katibu mkuu Knut, bwana Nyamu aliseama kuwa chama cha walimu kimeweka bayana matakwa yao waliyokubana na serikali mwaka 1997.
"marupurupu haya yote sharti yalipwe.Tumekwenda kwa wizara ya limu ya kuelezea malalmiko yetu,'' alisema bwana Nyamu.
"tunawaambia walimu kuwa katibu mkuu atawapa maagizo kuhusu watakachofanya wakati wa mgomo huu. Walimu waanze kwa kukabidhi majukumu yao katika shule zao leo.
Nyamu pia aliwataka walimu kuwaondoa watoto wao shuleni kwani walimu hawatakuwepo kuwafundisha.
''Kwa sasa tunaiacha serikali ifanye uamuzi , tutaketi chini na kusubiri,'' alisema Nyamu
''Wanachokitaka walimu ni pesa, na wale wanaomshauri rais wamwambie kuwa lazima walimi wapewe pesa kwani hawatazungumzia kingine ila marupurupu yao,'' alisema Sossion
Source: BBC
No comments:
Post a Comment