Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,anatangaza kuongeza muda wa kupokea maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2013/2014. Muda umeongezwa kutokana na sababu kubwa mbili:
i.Kubadilika kwa matokeo ya Wahitimu wa Kidato cha Nne
ii.Kuchelewa kwa majibu ya mitihani ya kuhitimu Kidato cha Sita.
Wahitimu wa Kidato cha Nne ambao walituma maombi yao ya kozi hapo awali (hadi tarehe 30/4/2013) na kupokelewa, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao mpya kwenye vituo vile vile wali kowasilisha maombi yao. Taarifa hizo ziainishe vitu vifuatavyo:
i.Jina kamili za muombaji
ii.Namba yake ya mtihani wa kidato cha Nne
iii.Matokeo yake mapya. ni vema kuwasilisha matokeo yaliyoko kwenye mtandao (internet) kwa vile ‘result Slips’ bado hazijatoka
iv.Kozi aliyochaguamara ya kwanza
v.Kozi anayoomba kwa matokeo mapya, kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye tangazo la Wizara
Kwa wahitimu wa Kidato cha Nne ambao hawakuomba hapo awali na wahitimu wa Kidato cha Sita, nafasi zinatangazwa kwa kozi zifuatazo:
(i) Afisa Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)
(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
(iii) Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)
(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician - off Campus) -Watajitegemea Malazi
(v) Optometria (Optometry)
(vi) Tabibu (Clinical Officer)
(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)
B.Kozi zangazi ya Cheti
(i) Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)
(ii) Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)
(iii) Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)
(iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)
C.Muda wa Mafunzo:
(i) Miaka mitatu kwa kozi za Stashahada
(ii)Miaka miwili kwa kozi za Ngazi ya cheti
D.Sifa za Muombaji:
Waombaji watarajali(Pre- service):
(i) Awe raia wa Tanzania
(ii) Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea
(iii) Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, katika masomo ya Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.
(iv) Kwa waombaji wa ngazi ya Cheti, cheti cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti.
Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(v) Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanahitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua 'E', kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(vi) Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.
E. Utaratibu wa kutuma maombi:
(i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na.Vii- viii) chini,
Waganga Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara. Pia zinapatikana kwenye tovuti ya wizara ambayo ni www.moh.go.tz.
(ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, itawasilishwa pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).
(iii) Malipo yaingizwe kwenye akaunti,‘
Health Service fund’, Account No. 0111- 030-12059 NBC–CORPORATE BRANCH.
(iv) Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti halisi ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.
(v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki (Pay in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.
(vi) Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.
(vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa Waratibu wa Kanda za Mafunzo, kupitia anuani za wakuu wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.
(viii) Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-
a)Mratibu wa Kanda ya Mashariki(Mikoa ya Morogoro na Pwani)- Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro.
b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora)- Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma
c) Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara) – Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.
d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga) – Chuo cha CEDHA, S.L.P. 1162, Arusha..
e) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.
f) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)- Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.
g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe , S.L.P.595, Dodoma.
h) Mratibu wa Kanda ya Zi wa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 1135, Mwanza.
i) Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili ,S.L.P 65005, Dar- es - salaam.
j) Mkuu wa Chuo cha Madaktari Wasaidizi - Tanga , S.L.P 5030, Tanga.
k) Mkuu wa Chuo cha Tabibu - Kibaha, S.L.P 30282, Kibaha
F.Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a) Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara ilyoainishwa hapo juu na mbao za matangazo Wizarani.
b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.
G. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Juni, 2013.
H.Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 14 Oktoba, 2013.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment