Thursday, June 6, 2013

TANGAZO LA AJIRA 2013/2014 - JESHI LA POLISI



                                                     TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ya Rasilimali watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLE), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi(Educational Psychology and Councelling),Takwimu, Lugha(Kiswahili/Kiingereza/Kifaransa/Kireno/Kiarabu), Usimamizi wa Programu za Maendeleo ya Jamii, Uhusiano wa Kimataifa, Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering), Uhandisi Kompyuta(Net Work, System Analyst, Data Base, Electronic & Telecommunications), Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma, Upangaji na Uendeshaji miradi, Jinsia na Watoto. Pia stashahada katika Usimamizi wa programu za maendeleo ya Jamii, Utunzaji kumbukumbu na Ukutubi.
Sifa za Muombaji:
  • Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 28.
  • Awe na tabia njema.
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa la jinai.
  • Awe na afya njema.
  • Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
  • Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
  • Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya na
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi.
Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.

3 comments:

  1. Anonymous6:22 PM

    nimekubali kuitumikia serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania

    ReplyDelete
  2. Anonymous6:26 PM

    nimekubali kuitumikia serikali kwa nguvu zangu zote na kwa hali na mali

    ReplyDelete
  3. Anonymous9:53 PM

    Jina thueni ally azizi mkazi wa tandika natamani sana kuwa mwanajeshi bcs ninamengi sana ya kuifanyia nchi yangu siwezi kuyasema ila nitakapo ingia nitaonesha kivitendo
    najua iposiku nitaingia tu nikimaliza kusoma chuo diploma yangu ya computer science
    ninamiaka 25

    ReplyDelete

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...