Mkuu wa majeshi nchini Libya Youseff al Man Gous amejiuzulu siku moja
baada ya ghasia mashariki mwa mji wa Benghazi kusababisha vifo vya watu
31.Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumamosi wakati waandamanaji
walipovamia kambi ya kundi la wanamgambo wanaojulikana Shield
wanaoiunga mkono serikali.Kundi hilo pia ndilo lililo na jukumu la kulinda
amani katika eneo hilo la Benghazi.Waandamanaji hao walikuwa wanataka
wanamgambo hao wakabidhi madaraka ya kiusalama kwa kikosi rasmi cha
usalama cha Libya na wasalimishe silaha zao. Bunge la kitaifa la Libya
limetangaza kujiuzulu kwa Youseff ambaye ameshutumiwa kwa kuchelewa
kuunda jeshi la kitaifa na kutangaza pia siku tatu za maombolezi.
Source:DW
No comments:
Post a Comment