Mahakama ya
Rufaa imeagiza kupelekwa majalada yote ya kesi inayomkabili Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Wilfred Lwakatare na mwenzake Lodvick Joseph.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama kutaka kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Kwa Mujibu
wa Msajili wa Mahakama Kuu, Projest Kahyoza, amepokea amri ya Mahakama
ya Rufani kuitisha jalada la Lwakatare lililopo Mahakama Kuu pamoja na
Kisutu na kuunganishwa kwa pamoja na kupelekwa mahakamani hapo.
Hatua hiyo
imefuatia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha ombi la
marejeo ya kutaka kuitishwa majalada ya kesi hiyo ili kuona uhalali wa
uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumfutia mashitaka ya ugaidi Lwakatare.
Machi 8,
mwaka huu, Lwakatare na mwenzake walipandishwa kizimbani mahakamani hapo
na kusomewa mashitaka manne likiwemo la ugaidi.
Hata hivyo,
Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimfutia
Lwakatare mashtaka matatu ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili na kubakiwa
na shitaka moja la kula njama kumnywesha sumu Msacky.
Uamuzi huo
ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Lawlance Kaduri baada ya kupitia
maombi yaliyowasilishwa na Mawakili wa Lwakatare na kusema kuwa DPP
hakuwa na uhalali wa kufuta kesi ya awali iliyofunguliwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18, mwaka huu na muda mfupi kuirudisha
mahakamani hapo kwa hakimu mwingine.
Source: CHADEMA's social media.
No comments:
Post a Comment