Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja
kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa
Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha
kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za
kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na
magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,”
alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini
Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza
kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika
watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George
Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na
Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa
hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na
kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za
kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la
litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni
hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo,
baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi
na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na
ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia
wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani.
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa
4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa
mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na
wakati huo.
Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi
Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako
Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa
barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya
Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.
Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni
wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe
watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa
Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.
Ulinzi hoteli za kitalii.
Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira
kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya
hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi
chumba.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli
zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta
kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.
Wamchongea JK.
Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani
(CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na
mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na
vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa
CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali
akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa
Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa Redio Kwizera.
Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation,
Absalom Kibanda.
Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.
Source:Mwananchi.Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.
Viongozi watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri
Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru
Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou
Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra
Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka)
na Mfalme wa Swaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana.
No comments:
Post a Comment