Taarifa ya Kukanusha Baadhi ya Matangazo katika Mitandao ya Kijamii
Ndugu Wandishi wa Habari, kwanza niwashukuru kwa kuitikia wito, nimewaita hapa kwa mambo mawili.Awali ya yote nianze kwa kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuelimisha umma juu ya masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii licha ya changamoto mbalimbali mnazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yenu.
Baada ya kusema
hayo, nianze kueleza nilichowaitia hapa nikitambua umuhimu wa nafasi
yenu katika jamii hususan katika kuelimisha umma kupitia vyombo vyenu.
Moja ya kazi za msingi za taasisi yetu kwa mujibu wa sheria
iliyoanzisha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kutangaza
nafasi wazi za Ajira kwa mujibu wa mahitaji.
Napenda kutoa rai kupitia kwenu na kwa wadau wetu wote watambue kuwa ni kosa kwa mtu au taasisi yoyote kuchukua matangazo ya Sekretarieti ya Ajira bila idhini na kuyafanyia marekebisho. Vile vile ni kosa kwa mujibu wa sheria kuandaa matangazo mbalimbali yanayohusiana na Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupotosha umma ilhali wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazozichapisha au kuziandika katika baadhi ya mitandao ya kijamii siyo halali na hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira.