Wanachama hao wamepatikana katika
mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na
Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan
Bahweje.
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya
Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani
Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti
wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama
wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya
Korogwe.
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada
ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa
wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za
vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na
muwekezaji.
Chanzo: CHADEMA Social media.
No comments:
Post a Comment