Hongera ndugu Bakari Machumu, Mhariri Mtendaji wa
Mwananchi Communications.
Napenda kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa
wasomaji wa magazeti ya Mwananchi na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC,
kukupongeza kwa kuteuliwa kwako kuwa Mhariri Mtendaji.
Magazeti
yenu yameonyesha uhuru mkubwa kwa kuandika habari za ukweli,
zilizofanyiwa utafiti na kwa utaalamu wa hali ya juu sana. Natumai chini
ya uongozi wako utaendelea kuenzi heshima hiyo ya magazeti ya Mwananchi
Communications.
... Changamoto kubwa sana kwa nji yetu ni
Ufisadi (rushwa) na Umasikini wa wananchi wetu licha ya kuwa tunaishi
kwenye nchi tajiri sana kwa rasilimali na watu pia. Sababu moja kubwa ya
kuendelea kwa hali hii ni ukosefu wa UWAJIBIKAJI. Vyombo vya habari ni
silaha kubwa sana ya kuhakikisha utamaduni wa uwajibikaji unaimarishwa
nchini kwetu. Hii ni kazi magazeti ya Mwananchi imefanya kwa muda mrefu,
lakini haitoshi. Juhudi lazima ziongezwe kuhakikisha kuwa viongozi wa
kisiasa wanajua kuwa matendo na maneno yao kamwe hatapita bila kuhojiwa
(Accountability and Answerability for actions and inactions).
Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, ambayo ina majukumu makubwa ya
kuimarisha uwajibikaji nchini, Napenda kukutia shime kuhakikisha kuwa
magazeti yenu yanashirikiana nasi kupambana na ufisadi na umasikini
nchini kwa kuimarisha uwajibikaji.
Nakutakia kazi njema wewe
binafsi na waandishi wote wa Mwananchi Communication.
Zitto
Kabwe
Mwenyekiti PAC
Bunge la Tanzania
Mwenyekiti PAC
Bunge la Tanzania
No comments:
Post a Comment