Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mjini Singida leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa
inanawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Ndugu Mwita Waitara ambaye ni
afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila
Mkumbo. Katika hukumu yake aliyeiosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao
Tundu Lissu Hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa
hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa
kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa. Aidha,
hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta
shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili
athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo
yamemuathiri. Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni
kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote
alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa,
alisema hakimu huyo.
Washtakiwa
walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. Kesi
hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa
kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara
kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.
Chanzo:CHADEMA Social Media.
No comments:
Post a Comment