Waandamanaji wachoma magurudumu kupinga hatua ya jeshi kuingia mji wa Kidal Kaskazini mwa Mali. |
Wanajeshi wa Ufaransa walioko katika eneo hilo wameripotiwa kufyatua risasi hewani kutawanya makundi hayo mawili.Wakati huo huo shirika la kutoa msaada, Islamic Relief, lenye makaazi yake nchini Uingereza limeonya kwamba licha ya mzozo kumalizika, eneo la kaskazini mwa Mali bado linakubwa na mkasa wa kibinadamu huku shule nyingi zikibaki kufungwa na masoko mengi kuahirishwa.
Mzozo uliopo kaskazini mwa mali umebuni kisiwa cha umaskini mkubwa katika eneo ambalo tayari limeathirika na kiangazi na uhaba wa chakula kabla ya vita kuzuka.
Shirika la Islamic Relief linasema watu milioni moja unusu sasa wanategemea chakula cha msaada , huku wengine milioni mbili wakikabiliwa na tishio la baa la njaa.
Nyingi ya barabara za kufanyia biashara kuelekea kaskazini zimefungwa kutokana na hali duni ya usalama na masoko kuahirishwa. Shirika la Islamic Relief linasema vita vimesababisha uharibifu wa mfumo wa usambazaji maji huku mabomba pamoja na visima vya maji vikiharibiwa kabisa.
Shirika hilo linasema kiwango cha mateso wanayokumbana nao wakaasi wa kaskazini mwa Mali kinafumbiwa macho. Limetowa wito kwa jamii ya kimataifa kufadhili mpango wa dharura wa kutoa msaada pamoja na miradi ya maendeleo ya kudumu.
Islamic Relief limesema kuwa kwa upande wake, limetowa chakula cha msaada pamoja na mbegu kwa wakulima.
Wapiganaji wa kundi la waasi la MNLA nchini Mali |
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment