Friday, July 26, 2013

HABARI KWA UFUPI KUTOKA MARA- KAHAWA KUNG'OLEWA,TABORA - USHIKINA WAUA,DAR- KESI YA DECI YAPIGWA KALENDA, NA MAKAMU WA RAIS ATOA ONYO.

USHIRIKINA WAUA TABORA:
Watu 3 wa ukoo mmoja wameuawa kwa kukatwa mapanga wakituhumiwa kuwa wachawi Wilayani Nzega, na msako waendelea na kuahidi vifo zaid.

KALENDA KESI YA DECI:
Hukumu dhidi ya viongozi wa Taasisi iliyoendesha mchezo haramu wa upatu ya DECI iliyopaswa kusomwa leo Kisutu imeahirishwa hadi Agosti 19.

KAHAWA YACHEFUA MARA:
Wakulima Tarime watishia kung'oa miche ya kahawa kupinga kulazimishwa kuuza kilo kwa Sh.700/= badala ya sh.1,500/= na wataka serikali iwatetee.

ONYO ARDHI:
Makamu wa Rais Mohamed Bilal aasa wakulima wasijichukulie sheria mkononi katika migogoro ya ardhi kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya MVIWATA leo.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...