Monday, January 28, 2013

LULU ARUDISHWA RUMANDE


Lulu akiwa na mwigizaji mwenzake Ray kabla ya kwenda mahabusu.

Katika hali isiyo ya kwawaida mwigizaji Elizabert Michael a.k.a Lulu amerudishwa rumande baada ya taratibu za dhamana kutokamilika. 
Lulu akipanda gari kurudishwa rumande
Lulu akitoka mahakamani

Kwa mujibu wa mhabarishaji aliyekuwa mahakamani hapo amesema Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa Mahakama ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo,hivyo dhamana yake inaweza kuwezekana keho.
Awali,Mahakama Kuu ya Tanzania iliweka wazi masharti ya dhamana ya msanii 
  huyo ambayo ilikuwa ni pamoja na:
  • Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
  • Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
  • Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
  • Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

HABARI ZILIZOVUNJIKA:LULU APEWA DHAMANA


Habari zilizopatikana hivi punde kutoka mahakamani zinasema kuwa Lulu amepewa dhamana na Mahakama kuu ya Tanzania baada ya mawakili wanaomtetea Lulu kuwasilisha ombi la dhamana mahakamani hapo.
Mawakili hao ambao ni Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliiomba mahakama hiyo itoe dhamana haraka kwakuwa mteja wao amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Ikumbukwe kuwa Elizabeth Michael anakabiliwa na kosa la kumuua mwigizaji mwenzake Kanumba bila kukusudia tukio lililotokea mnamo 07/04/2012


WIZARA YA AFYA NA AFYA YA JAMII. 
Wizara ya afya na ustawi wa jamii katika kuhakikisha kuwa inaboresha afya ndani ya jamii, imetangaza nafasi za mafunzo ya idara ya afya katika vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo. Nawaomba watanzania wenzangu tumia nafasi hii kuomba nafasi hizo.
Maelekezo yote kuhusiana na nafasi hizo yapo hapa chini kwenye tangazo kao.

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

         MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2013/14




Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara kwa mwaka wa masomo 2013/2014.



1.      Kozi zinazotangazwa ni:  



A.    Ngazi ya Stashahada:

(i)             Afisa Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)

(ii)           Fiziotherapia (Physiotherapy)

(iii)          Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)

(iv)          Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)

(v)           Optometria (Optometry)

(vi)          Tabibu (Clinical Officer)

(vii)        Tabibu Meno (Dental Therapist)

(viii)       Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)



B.    Ngazi ya Cheti



(i)             Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)

(ii)           Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)

(iii)          Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)

(iv)          Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)



C.    Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa (Distance Learning) kwa wale waliohitimu mafunzo ya Tabibu Msaidizi mwaka 2009.



2.     Muda wa Mafunzo:

(i)             Miaka mitatu kwa kozi za Stashahada

(ii)           Miaka miwili kwa kozi za Ngazi ya cheti

 


3.     Sifa za Muombaji:

Waombaji watarajali (Pre-service):

(i)             Awe raia wa Tanzania

(ii)           Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea

(iii)          Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  katika  masomo ya Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada . Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.

(iv)          Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.

(v)           Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua ‘E’,  kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha  mtihani.

(vi)          Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.





Waombaji wa Mafunzo ya Masafa (Distance learning:

  1. Wanaotakiwa kujiunga na Bridging course kabla ya kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya waganga wasaidizi vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.

  1. Tabibu wasaidizi (NTA 5) Wanaotakiwa kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne.

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Tabibu wasaidizi (NTA 5) mwaka 2009.

4.     Utaratibu wa kutuma maombi:

(i)    Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, Waganga Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara.

(ii)  Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, iwasilishwe pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).

(iii)Malipo  yaingizwe kwenye akaunti ,Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.

(iv)Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti halisi ya malipo ya Benki,  inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.

(v)  Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay  in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.

(vi)Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.

(vii)      Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa Katibu Mkuu,  wizara ya afya na ustawi wa jamii,kupitia anwani za wakuu wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.

(viii)    Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

a)      Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro.

b)     Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma

c)      Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.

d)     Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha CEDHA, S.L.P.1162, Arusha..

e)      Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.

f)       Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.

g)     Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe, S.L.P. 595, Dodoma.

h)     Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza.

i)      Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam.



5.     Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:

a)     Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara na mbao za matangazo Wizarani.  

b)     Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.



6.     Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2013.

7.     Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2013.



Imetolewa na:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

Dar es Salaam

Monday, January 21, 2013

UKUTA WA KITUO CHA MABASI UBUNGO WAANGUKIA MAGARI ZAIDI YA 24.
Muonekano wa namna ukuta ulivyoangukia magari
Katika hali ya kushangaza,magari zaidi ya 24 yameangukiwa na ukuta wa stendi ya mabasi Ubungo wakati mkandarasi akijaribu kubomoa ukuta huo kwa matengenezo.
Gari aina na suzuki likiwa nyang'anyang'a

Chanzo cha habari hii kinasema kuwa inasemekana kuna na majeruhi waliotokana na ajari hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Dar wakiwa wanashangaa ajari ilivyotokea.

Gari ndogo ikiwa hoi bini taabani.
Swali langu hapa ni "nani atakayewajibika na fidia?"


Thursday, January 17, 2013

HUU NI UZEMBE KAZINI USIO VUMILIKA.
Hiki ni kituo cha Afya cha Saba saba katika Manispaa ya Morogoro ambacho ni mojawapo ya ofisi za Serikali.Tarehe 13/11/2012 nilifika katika kituo hiki na kukuta BENDERA YA TAIFA ikiwa inapepea mida ya saa 1 usiku,nikasema labda yule mlinzi mwenye wajibu wa kuishusha anadharula.Lakini kitu cha kushangaza jana  tarehe 16/01/2013 usiku minamo saa 1 usiku pia bendera hiyo imekutwa bado inapepea wakati najua fika kuwa bendera inatakiwa kushushwa saa 12 jioni.

Nimekaa pale mpaka bendera hiyo imekuja kushushwa saa 1.28 usiku.


SWALI langu,ni je,taratibu za kushushwa kwa bendera zimebadilika au ni uzembe tuu wa watu wasiojali kazi zao.

Wednesday, January 16, 2013

OKWI HUYOOOOOOO TUNISIA


Picha ya Okwi akiwa anamiliki mpira.
  Emmanuel Okwi 
Hi guys thanks to God the deal is done.. Am officially a player of Etoile Sportive Du Sahel, it's really a new challenge and a big step for me in my carrier.. Let me take this chance to thank all Simba fans and officials for the support u gave me.. U were really special to me, god bless u all.. Alluta continua..
Hayo ni maneno yake Okwi aliyoyaandika katika ukurasa wake wa Facebook. 
Na kwa upande wa Simba sport club,kutokana na taarifa walizozisambaza kwa wapenzi wa timu hiyo kwa njia ya ujumbe mfupi leo hasubuhi ni kama ifuatavyo:  
"Hatimaye uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumuuza mshambuliaji wake Mganda Emmanueli Okwi kwa klabu ya Eoile du sahel ya Tunisia kwa ada ya dola laki 3" 
Namtakia kila la kheri huko aendako.

Tuesday, January 8, 2013

UDHAIFU WA WAKANDARASI WAZAWA KATIKA KAZI ZA UJENZI.
Barabara ya IPO IPO - KIHONDA MAGOROFANI

Umekuwa ni wimbo kuwa kazi nyingi za ujenzi wanapewa wakandarasi kutoka nchi za nje wakati wakandarasi wazawa wakinyimwa kazi.Malalamiko haya yanasikika kila mahali lakini je,sisi wazawa kazi zetu zinaridhisha???.
 
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina mkakati mzuri wa kuboresha barabara zake ili ziweze kupitika kirahisi ili kurahisisha  mawasiliano katika maeneo mbali mbali.Miongoni mwa barabara hizo ni ile ya IPOIPO - KIHONDA MAGOROFANI ambayo ilijengwa kwa kiwango cha lami.Ili kusikiliza kilio cha wakandarasi wazawa kuwa hawapewi kazi Manispaa ikampa kazi mkandarasi aitwaye:MAGINGA BUSINESS HOLDINGS CO Ltd,S.L.P. 1523,DODOMA.





Lakini kazi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa MHANDISI WA MANISPAA YA MOROGORO,kitu cha kushangaza nikwamba tangu kazi hii ikamilike haina miezi hata mitatu (3) lakini kwa mvua kidogo zilizonyesha tarehe 05/01/2013 zimebomoa barabara hii vibaya sana kiasi cha zile 'slabs' kuondoshwa na mvua pembezoni mwa barabara.

Swali langu ni je,barabara hii itadumu kweli?
Watanzania tuacheni kulalamika tu,tuwajibike na tuwe makini na kazi tunazofanya ili tuweze kuuza soko letu kitaifa na kimataifa.

Monday, December 31, 2012

HERI YA MWAKA MPYA 2013.

MWENYEZI MUNGU MWENYE KUWEZA KILA JAMBO,AMEWEZA KUKUONGOZA VIZURI MPAKA SASA UNAPUMUA. Una kila sababu ya kumshukuru kwa kila jambo.Niwengi waliuanza huu mwaka wa 2012 lakini katikati safari zao zikakatishwa na uhai wao kuweza kuchukuliwa.

Jiulize kwa mwaka 2012 umefanya nini la kumtukuza mwenyezi mungu,umefanya nini la kuisaidia jamii.Ukishafanya tathimini hiyo jipe jibu na kuweza kujikosoa.

Wengi tunalalamika kuwa hatuna kitu,lakini kusaidia ni moyo sio utajiri.Mtu mwingine unaweza kumsaidia mawazo na akaweza kukwamuka kimaisha.

Nawaomba tupendane wote madamu tunaishi,sote ni ndugu.


DAR ES SALAAM YATOLEWA KAFARA KWENYE DIJITALI.

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof.Makame Mbarawa.


MKOA wa Dar es Salaam saa 6 kamili usiku wa leo unakuwa wa kwanza kuzimiwa mitambo ya analojia ya utangazaji wa televisheni kwa ajili ya kupokea mfumo mpya wa digitali.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa katika hotuba yake ya jana kuashiria uzimaji wa mitambo ya analojia, alisema uzimaji kwa zamu unalenga kuepusha usumbufu kwa wananchi wa Tanzania.

Mbarawa alisema kuwa mchakato huo wa uzimaji wa mitambo utafanyika kama ifuatavyo: Januari 31, 2013 Dodoma na Tanga. Mkoani Mwanza Februari 28, 2013 na Kilimanjaro (Moshi) na Arusha Machi 31, 2013.

Mkoa wa saba kuingia kwenye mfumo wa digitali utakuwa Mbeya ambao mitambo itazimwa Aprili 30, 2013. Utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwa maeneo yenye matangazo ya digitali na kwa yasiyo na miundombinu ya digitali hayatazimwa.

Taarifa ya Waziri inaonesha kwamba miundombinu ya mitambo ya digitali imeenea katika mikoa minane pekee. Mabadiliko hayo yanahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti, waya (cable) na redio.

Aidha imeelezwa kwamba watoa huduma za miundombinu ya digitali wamejipanga kusimika mitambo hiyo katika mikoa mingine minane ndani ya miezi minane ijayo.
Lakini kwa upande wa pili wa shilingi,baadhi ya wananchi wanalalamikia ving'amuzi vingine vunakatakata sana mawasiliano,lakini naona ni changamoto.


Friday, December 28, 2012

UZURI NA MAAJABU YA BUKOBA

Bukoba ni sehemu mojawapo ambayo kila mmoja anapenda akaishi kutokana na uzuri wake.Kihistoria,Bukoba ni sehemu miongoni mwa sehemu barani Afrika ambayo ilitawaliwa na Utawala wa Machifu (WAKAMA).Miongoni mwa machifu hao ni Mukama Lukamba ambaye alikuwa "Chief" wa Kyamutwara makao makuu yake ni Kabale,kata ya Karabagaine.

Nyumbani kwa Mukama Lukamba.



Kwa Wakama  hawa kulikuwa na mahakama (GOMBOLOLA) ambazo zilikuwa zinatumika kuhukumu waarifu wote waliokuwa wanaletwa mahakamani hapo.

Chief Lwaijumba local court
Mahakama ya Mukama Lwaijumba ambapo waarifu walikuwa wanahukumiwa.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo wote waliokuwa wanaadhibiwa kwa kunyongwa sehemu inayoitwa Mlima wa Lyankumbi ulioko Itahwa walipokuwa wanaachiwa na kuporomokwa hadi bondeni.
Mlima Lyankumbi ampako waarifu walikuwa wanaanyongwa.

Pamoja ni hayo,Kabale kuna pango ambalo lilitumika kwa wananchi kujificha wakati wa vita ya Kagera.Pango hilo lina urefu usiopungua kilometa 3.Pango hili la maajabu lipo katika mlima Rwamrumba.
Picha zifuatazo ni picha zinazoonesha pango la maajabu.




Mnamo miaka ya 1977 hadi 1979 kulikuwa na vita ya Kagera,vita hivi vilifanyika hasa maeneo ya Mutukura,Bunazi na Kyaka.Miongozi mwa uharibifu uliofanyika wakati wa vita ni Kuunguzwa kwa kiwanda cha sukari cha Kagera,Kuunguzwa kwa makanisa pamoja na mashule.
Picha zifuatazo ni baadhi tu ya picha zinazoonesha uharibifu uliofanywa na Nduli Iddi Amini -DADA kwa kuunguza kanisa la Kyaka.


Kanisa la Kyaka lililoungua.







LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...