Monday, December 31, 2012


DAR ES SALAAM YATOLEWA KAFARA KWENYE DIJITALI.

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof.Makame Mbarawa.


MKOA wa Dar es Salaam saa 6 kamili usiku wa leo unakuwa wa kwanza kuzimiwa mitambo ya analojia ya utangazaji wa televisheni kwa ajili ya kupokea mfumo mpya wa digitali.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa katika hotuba yake ya jana kuashiria uzimaji wa mitambo ya analojia, alisema uzimaji kwa zamu unalenga kuepusha usumbufu kwa wananchi wa Tanzania.

Mbarawa alisema kuwa mchakato huo wa uzimaji wa mitambo utafanyika kama ifuatavyo: Januari 31, 2013 Dodoma na Tanga. Mkoani Mwanza Februari 28, 2013 na Kilimanjaro (Moshi) na Arusha Machi 31, 2013.

Mkoa wa saba kuingia kwenye mfumo wa digitali utakuwa Mbeya ambao mitambo itazimwa Aprili 30, 2013. Utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwa maeneo yenye matangazo ya digitali na kwa yasiyo na miundombinu ya digitali hayatazimwa.

Taarifa ya Waziri inaonesha kwamba miundombinu ya mitambo ya digitali imeenea katika mikoa minane pekee. Mabadiliko hayo yanahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti, waya (cable) na redio.

Aidha imeelezwa kwamba watoa huduma za miundombinu ya digitali wamejipanga kusimika mitambo hiyo katika mikoa mingine minane ndani ya miezi minane ijayo.
Lakini kwa upande wa pili wa shilingi,baadhi ya wananchi wanalalamikia ving'amuzi vingine vunakatakata sana mawasiliano,lakini naona ni changamoto.


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...