Tuesday, November 6, 2012

VIWANDA VYA MOROGORO VYATELEKEZWA.
Zilikuwa ni juhudi za Mwl.J.K.Nyerere za kujenga viwanda hasa eneo la Morogoro lakini cha kushangaza viwanda karibu vyote vimekufa hasa baada ya kubinafsishwa.
Mpaka sasa viwanda ambavyo vinahali mbaya ni kiwanda cha viatu cha MOROSHOE na kiwanda cha bidhaa zinazotokana na ngozi LEATHER GOODS.Viwanda hivi havifanyi kazi zaidi ya kuanza kuporomoka na kuanguka.
Wito wangu kwa serikali ni kuvifufua viwanda hivi ili vifanye kazi kama vilivyo kusudiwa ikizingatiwa kuwa ni fedha za kodi za wananchi ndo zilizotumika kujengea viwanda hivi.
FAHARI YA MOROGORO ISIYOTHAMINIWA.
Mji wa Morogoro umezungukwa na milima ya Uluguru ambayo ina vivutio mbali mbali ikiwa ni pamoja na wanyama adimu aina ya MBEGA.Milima hii ni tegemeo kubwa la vyanzo vya maji katika mikoa ya Morogoro,Pwani na Dar es salaam.Bwawa la Mindu ambalo linategemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro linaloundwa na mito mitano yote inaanzia katika safu za milima ya Uluguru.
Milima hii kipindi cha miaka ya sabini maji yalikuwa yakitiririka milimani lakini kama inavyoonekana watu wameivamia milima hii na kuendesha shughuri mbali mbali kama kilimo na uwindaji wa wanyama.Kutokana na uharibifu huo kwa sasa hali ya maji inazidi kuwa mbaya.
Jamani tushirikiane wote katika kurudisha hali ya milima hii ya Uluguru.
AFYA
Sehemu nyingi za kazi afya za watendaji wa kazi hazijaliwi.Kinachofanyika hapo ni mwajiri kuona kazi yake imekamilika lakini mazingira ya kukamilika kwa kazi hiyo hayafatilii na kuyafanyia kazi.Kutokana na Sheria ya Afya na Usalama kazini (The Occupational Health and Safety Act,2003) kifungu namba 62,wafanyakazi wote wanatakiwa kupewa vitendea kazi na vifaa vya kujikinga na madhara ya kazi wanazozifanya...
Expand this post »
UKATAJI MITI OVYO.
Hili ni kanisa mojawapo hapa Manispaa ya Morogoro ambalo linatumia magogo kama viti vya kukalia waumini wake wawapo kanisani.Ili kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali,bora zingepasuriwa mbao harafu tukatengeneza mabenchi kuliko kukata magogo kama inavyoonekana.
Hili ni kanisa la SAUTI YA UPONYAJI la NABII JOSHUA lililo Kihonda Viwandani karibu na Kiwanda cha Ngozi.
UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
Matumizi ya nishati ya misitu katika viwanda vyetu hata Morogoro yanazidi kuongezeka kiasi kwamba viwanda vingine vinatumia kuni kuendeshea mitambo ili kukwepa gharama za umeme.Kiwanda kimojawapo kinachotumia  kuni kuendeshea mitambo yake ni 21st Century Textiles Ltd.
Haya ni magogo yaliyorundikwa kusubiria kutumika.Jamani,kutengeneza msitu inaweza kutuchukua muda si chini ya miaka kumi lakini ufyekaji unaweza kufanyika ndani ya siku kadhaa tu.Kibaya zaidi hawa wanaokata miti ukiwauliza wamepanda mingapi utaambiwa hawajapanda mti hata mmoja.
Watanzania tuamke,tutunze mazingira yetu ili hata vizazi vijavyo vikute hizi rasilimali tulizonazo.
INDUSTRIAL WASTE WATER MANAGEMENT.
Morogoro ni mji mmojawapo ambao Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere aliufanya uwe wa viwanda vingi ambavyo vilikuwa vya Tumbaku,Ngozi,Maturubai,Nguo,Magunia,Viatu n.k.Baada ya ujenzi wa viwanda hivi palijengwa mabwawa ya majitaka ya viwandani mahususi kwa kuhudumia hasa Kiwanda cha Selamic,Moroshoe na Canvas.Mabwawa hayo  yalikuwa chini ya miliki ya TLAI,lakini baada ya viwanda kubinafsishwa mabwawa hayo yakawa hayana mwangalizi kama inavyoonekana.
Ombi langu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,iangalie uwezekano wa kuyakarabati mabwawa haya ili kunusuru afya za wananchi.
4 photos
DUMPING SITE MOROGORO MUNICIPAL.
Hii ndo hali halisi ya dampo la Manispaa ya Morogoro ambalo halijaliwi na wala halifanyi kazi yake kama ilivyokusudiwa .Taka ngumu zinamwagwa hadi getini kiasi kwamba hata gari la taka ngumu haliwezi kuingia kumwaga taka.Kibaya zaidi taka hizo zinachomwa hapo hapo zilipo mpaka moto unatoka nje ya fensi ya dampo hilo kama inavyoonekana.Swali langu kwa Halmashauri ya manispaa ya Morogoro Idara ya afya ,je,hali hii wanaijua? Kama wanaijua hatua gani zimechukuliwa.Badala ya kuwa contolled tipping inakuwa crude dumping.Tafakari,chukua hatua.
UKAME! UKAME! UKAME! UKAME!
Hali ya maji Morogoro inazidi kuwa mbaya baada ya Bwawa la Mindu kupungua kina cha maji kwa kasi baada ya ukame kuendelea kukausha maji.Hii yote inatokana na uchafuzi wa mazingira.Hivi ndivyo bwawa la Mindu linavyoonekana.
MATUNDA.
Morogoro inasifika kwa kuwa na matunda aina mbali mbali ya kutosha ambayo yanapatikana maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro.
Changamoto kubwa ninayoiona hapa ni utunzaji wa matunda hayo yanayoletwa mjini.Yanamwagwa tu chini bila kujali usalama wake swala ambalo linaweza kuleta madhara kiafya kwa walaji.Wafanya biashara wa matunda wawe wanafatiliwa kwa ukaribu ili kuweza kuwadhibiti kutoharibu ubora wa matuda hayo.Wafanyabiashara hawa wamekutwa wamemwaga matunda chini eneo la Sume Mwembesongo.
BARAZA LA WAFANYAKAZI.
Hili ni baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) lenye jumla ya wajumbe 42.Baraza hili lina majukumu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwatetea wafanyakazi na kupitisha makisio ya bajeti za Mamlaka.
Baraza hili lilizinduliwa rasmi tarehe 13/06/2012 na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha wafanya kazi wa serikali kuu na Afya (TUGHE) Dr.Mrutu.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...