Monday, July 1, 2013
MISRI HALI TETE,RAIS ATAKIWA KUJIUZULU HADI KUFIKiA KESHO.
Umoja wa vyama vya upinzani unaompinga Rais Mohammed Morsi wa Misri, umemtaka Rais huyo kujiuzulu hadi kufikia kesho au atarajie uasi zaidi,na hii ikiwa ni mwaka mmoja tangu
aingie madarakani. Siku ya jana ilimalizika kwa
kuwashuhudia watu wakimiminika mitaani kwenye mji
mkuu, Cairo. Wapinzani wanalituhumu kundi la Udugu wa
Kiislamu la Rais Morsi kwa kuyateka mapinduzi ya umma,
kupitia ushindi kwenye uchaguzi, kujilimbikizia madaraka
na kutaka kuweka Sharia ya Kiislamu. Waandamanaji
wengine wanasema wamevunjwa moyo na mgogoro wa
kiuchumi. Maafisa wa usalama wanasema ofisi tatu za
chama cha Udugu wa Kiislamu zilichomwa moto na
waandamanaji kwenye jimbo la Nile Delta. Zaidi ya wafuasi
20,000 wa Rais Morsi pia walikusanyika karibu na kasri ya Rais mjini Cairo kumuunga mkono kiongozi huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment