Wednesday, January 30, 2013

MVUA ZILIZONYESHA JANA MOROGORO


Bwawa la Mindu

Jana kulinyesha mvua kubwa sana Mjini Morogoro kiasi cha kuwasababishia madhara baadhi ya wakazi wa Manispaa wanaoishi mabondeni ikiwa ni pamoja na kusombwa kwa baadhi ya nyumba.
Mkazi wa Morogoro akifurahi baada ya mvua kunyesha hiyo jana
Lakini pamoja na kunyesha kwa mvua hizo hali ya maji katika  bwawa la Mindu haikubadilika sana maana mpaka kufika leo saa 9.30 mchana maji yalikuwa yameongezeka kwa kiasi cha sentimeta sita (sm 6),lakini kiasi cha maji yanayoingia bwawani kinaweza kuwa kimebadilika na kuongezeka kufika kesho asubuhi maana mito inaendelea kuingiza maji bwawani.

TAIFA STARS KUKIPIGA NA CAMEROON

Kikosi cha Taifa stars

Timu ya taifa mpira wa miguu ya Tanzania Taifa stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Cameroon mchezo utakaopigwa Februari 06,2013 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 11 kamili jioni.
Kikosi cha Cameroon kinatarajiwa kuwasili hapa nchini tarehe 03 Februari,2013 kwaajiri ya mtanange huo.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo upo katika calenda ya FIFA,hivyo matokeo ya mchezo huo yanatumika kutuweka kwenye nafasi za viwango vya FIFA.

UKAME MKALI WAIKUMBA MOROGORO

Bwawa la Mindu likiwa limekauka kwa ukame

Hali ya mji wa Morogoro inazidi kuwa mbaya baada ya kutonyesha mvua kwa muda mrefu.Ukame huu umepelekea maji katika bwawa la maji la Mindu kukauka na kupungua kina cha maji kwa meta 2 (2m)
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mjisafi na Usafi wa mazingira Morogoro wamefanya ziara ya kutembelea vyanzo vya maji na kujionea upungufu wa maji .
Wajumbe wa Balaza la Wakurugenzi wa MORUWASA pamoja na watendaji wakiwa wanaangalia jinsi bwawa lilivyokauka.

Katika kujumuisha ziara hiyo,Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa amewasihi wananchi wote pamoja na wanasiasa kushirikiana katika suala zima la utunzaji wa mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita amesema suala hili la uharibifu wa Mazingira linasababisha "mgao wa maji ndani ya mgao" kutokana na upungufu huo wa maji.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita







Monday, January 28, 2013

LULU ARUDISHWA RUMANDE


Lulu akiwa na mwigizaji mwenzake Ray kabla ya kwenda mahabusu.

Katika hali isiyo ya kwawaida mwigizaji Elizabert Michael a.k.a Lulu amerudishwa rumande baada ya taratibu za dhamana kutokamilika. 
Lulu akipanda gari kurudishwa rumande
Lulu akitoka mahakamani

Kwa mujibu wa mhabarishaji aliyekuwa mahakamani hapo amesema Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa Mahakama ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo,hivyo dhamana yake inaweza kuwezekana keho.
Awali,Mahakama Kuu ya Tanzania iliweka wazi masharti ya dhamana ya msanii 
  huyo ambayo ilikuwa ni pamoja na:
  • Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
  • Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
  • Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
  • Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.

HABARI ZILIZOVUNJIKA:LULU APEWA DHAMANA


Habari zilizopatikana hivi punde kutoka mahakamani zinasema kuwa Lulu amepewa dhamana na Mahakama kuu ya Tanzania baada ya mawakili wanaomtetea Lulu kuwasilisha ombi la dhamana mahakamani hapo.
Mawakili hao ambao ni Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliiomba mahakama hiyo itoe dhamana haraka kwakuwa mteja wao amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Ikumbukwe kuwa Elizabeth Michael anakabiliwa na kosa la kumuua mwigizaji mwenzake Kanumba bila kukusudia tukio lililotokea mnamo 07/04/2012


WIZARA YA AFYA NA AFYA YA JAMII. 
Wizara ya afya na ustawi wa jamii katika kuhakikisha kuwa inaboresha afya ndani ya jamii, imetangaza nafasi za mafunzo ya idara ya afya katika vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo. Nawaomba watanzania wenzangu tumia nafasi hii kuomba nafasi hizo.
Maelekezo yote kuhusiana na nafasi hizo yapo hapa chini kwenye tangazo kao.

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

         MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2013/14




Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara kwa mwaka wa masomo 2013/2014.



1.      Kozi zinazotangazwa ni:  



A.    Ngazi ya Stashahada:

(i)             Afisa Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)

(ii)           Fiziotherapia (Physiotherapy)

(iii)          Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)

(iv)          Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)

(v)           Optometria (Optometry)

(vi)          Tabibu (Clinical Officer)

(vii)        Tabibu Meno (Dental Therapist)

(viii)       Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)



B.    Ngazi ya Cheti



(i)             Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)

(ii)           Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)

(iii)          Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)

(iv)          Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)



C.    Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa (Distance Learning) kwa wale waliohitimu mafunzo ya Tabibu Msaidizi mwaka 2009.



2.     Muda wa Mafunzo:

(i)             Miaka mitatu kwa kozi za Stashahada

(ii)           Miaka miwili kwa kozi za Ngazi ya cheti

 


3.     Sifa za Muombaji:

Waombaji watarajali (Pre-service):

(i)             Awe raia wa Tanzania

(ii)           Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea

(iii)          Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  katika  masomo ya Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada . Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.

(iv)          Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.

(v)           Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua ‘E’,  kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha  mtihani.

(vi)          Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.





Waombaji wa Mafunzo ya Masafa (Distance learning:

  1. Wanaotakiwa kujiunga na Bridging course kabla ya kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya waganga wasaidizi vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.

  1. Tabibu wasaidizi (NTA 5) Wanaotakiwa kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)

               i.         Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne.

              ii.         Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Tabibu wasaidizi (NTA 5) mwaka 2009.

4.     Utaratibu wa kutuma maombi:

(i)    Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, Waganga Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara.

(ii)  Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, iwasilishwe pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).

(iii)Malipo  yaingizwe kwenye akaunti ,Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.

(iv)Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti halisi ya malipo ya Benki,  inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.

(v)  Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay  in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.

(vi)Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.

(vii)      Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa Katibu Mkuu,  wizara ya afya na ustawi wa jamii,kupitia anwani za wakuu wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.

(viii)    Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

a)      Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro.

b)     Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma

c)      Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.

d)     Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha CEDHA, S.L.P.1162, Arusha..

e)      Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.

f)       Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.

g)     Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe, S.L.P. 595, Dodoma.

h)     Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza.

i)      Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam.



5.     Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:

a)     Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara na mbao za matangazo Wizarani.  

b)     Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.



6.     Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2013.

7.     Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2013.



Imetolewa na:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

Dar es Salaam

Monday, January 21, 2013

UKUTA WA KITUO CHA MABASI UBUNGO WAANGUKIA MAGARI ZAIDI YA 24.
Muonekano wa namna ukuta ulivyoangukia magari
Katika hali ya kushangaza,magari zaidi ya 24 yameangukiwa na ukuta wa stendi ya mabasi Ubungo wakati mkandarasi akijaribu kubomoa ukuta huo kwa matengenezo.
Gari aina na suzuki likiwa nyang'anyang'a

Chanzo cha habari hii kinasema kuwa inasemekana kuna na majeruhi waliotokana na ajari hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Dar wakiwa wanashangaa ajari ilivyotokea.

Gari ndogo ikiwa hoi bini taabani.
Swali langu hapa ni "nani atakayewajibika na fidia?"


Thursday, January 17, 2013

HUU NI UZEMBE KAZINI USIO VUMILIKA.
Hiki ni kituo cha Afya cha Saba saba katika Manispaa ya Morogoro ambacho ni mojawapo ya ofisi za Serikali.Tarehe 13/11/2012 nilifika katika kituo hiki na kukuta BENDERA YA TAIFA ikiwa inapepea mida ya saa 1 usiku,nikasema labda yule mlinzi mwenye wajibu wa kuishusha anadharula.Lakini kitu cha kushangaza jana  tarehe 16/01/2013 usiku minamo saa 1 usiku pia bendera hiyo imekutwa bado inapepea wakati najua fika kuwa bendera inatakiwa kushushwa saa 12 jioni.

Nimekaa pale mpaka bendera hiyo imekuja kushushwa saa 1.28 usiku.


SWALI langu,ni je,taratibu za kushushwa kwa bendera zimebadilika au ni uzembe tuu wa watu wasiojali kazi zao.

Wednesday, January 16, 2013

OKWI HUYOOOOOOO TUNISIA


Picha ya Okwi akiwa anamiliki mpira.
  Emmanuel Okwi 
Hi guys thanks to God the deal is done.. Am officially a player of Etoile Sportive Du Sahel, it's really a new challenge and a big step for me in my carrier.. Let me take this chance to thank all Simba fans and officials for the support u gave me.. U were really special to me, god bless u all.. Alluta continua..
Hayo ni maneno yake Okwi aliyoyaandika katika ukurasa wake wa Facebook. 
Na kwa upande wa Simba sport club,kutokana na taarifa walizozisambaza kwa wapenzi wa timu hiyo kwa njia ya ujumbe mfupi leo hasubuhi ni kama ifuatavyo:  
"Hatimaye uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumuuza mshambuliaji wake Mganda Emmanueli Okwi kwa klabu ya Eoile du sahel ya Tunisia kwa ada ya dola laki 3" 
Namtakia kila la kheri huko aendako.

Tuesday, January 8, 2013

UDHAIFU WA WAKANDARASI WAZAWA KATIKA KAZI ZA UJENZI.
Barabara ya IPO IPO - KIHONDA MAGOROFANI

Umekuwa ni wimbo kuwa kazi nyingi za ujenzi wanapewa wakandarasi kutoka nchi za nje wakati wakandarasi wazawa wakinyimwa kazi.Malalamiko haya yanasikika kila mahali lakini je,sisi wazawa kazi zetu zinaridhisha???.
 
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina mkakati mzuri wa kuboresha barabara zake ili ziweze kupitika kirahisi ili kurahisisha  mawasiliano katika maeneo mbali mbali.Miongoni mwa barabara hizo ni ile ya IPOIPO - KIHONDA MAGOROFANI ambayo ilijengwa kwa kiwango cha lami.Ili kusikiliza kilio cha wakandarasi wazawa kuwa hawapewi kazi Manispaa ikampa kazi mkandarasi aitwaye:MAGINGA BUSINESS HOLDINGS CO Ltd,S.L.P. 1523,DODOMA.





Lakini kazi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa MHANDISI WA MANISPAA YA MOROGORO,kitu cha kushangaza nikwamba tangu kazi hii ikamilike haina miezi hata mitatu (3) lakini kwa mvua kidogo zilizonyesha tarehe 05/01/2013 zimebomoa barabara hii vibaya sana kiasi cha zile 'slabs' kuondoshwa na mvua pembezoni mwa barabara.

Swali langu ni je,barabara hii itadumu kweli?
Watanzania tuacheni kulalamika tu,tuwajibike na tuwe makini na kazi tunazofanya ili tuweze kuuza soko letu kitaifa na kimataifa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...