Monday, March 25, 2013

GARI LAFUNGA BARABARA YA DAR - MORO KWA MASAA KADHAA RUVU BAGAMOYO

Askari polisi wakisimamia usalama
Gari roli lenye namba za usajiri T451ARW liligongana na roli lenye namba za usajiri T475BNA eneo la Ruvu Wilaya ya Bagamoyo na kusababisha foleni kwa magari yanayotoka chalinze kwenda Dar na kutoka dar kwenda Chalinze.Foleni hiyo ilidumu kwa takribani muda usiopungua masaa matatu.
Foleni baada ya gari kuziba barabara
Kivutio zaidi ni pale vijana wapao 7 waliokuwa wakipakiza chokaa huku wakiwa hawana hata mask za kuzuia vumbi lisiwadhuru.
Vijana wakipakia chokaa




MAN UNITED YAFANIKIWA KUMSAINISHA BEKI WA KATI EZEQUIEL GARAY KUTOKA BENFICA.

Timu ya Manchester United imwfanikiwa kumsainisha Ezequiel Garay kutoka Benfica kwa kitita cha Paundi Mil.17.Man U na Benfica zimekubaliana kuwa Garay atahamia Old Traford majuma machache yajayo ili aweze kuichezea timu hiyo wakati wa kiangazi.

Garay mwenye umri wa miaka 26 aliyezaliwa Bosario tarehe 10.10.1986 amekuwa akizungumziwa mara kwa mara kuwa anawaniwa na Mashetani wekundu.

Thursday, March 21, 2013

KIKAO CHA KAMATI YA MAZINGIRA CHAFANYIKA CHINI YA NAIBU SPIKA UBELGIJI

Mheshimiwa Naibu Spika akiwasilisha taarifa kwenye kikao kinachoendelea Ubelgiji.
 Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jobu Ndugai ameongoza kikao cha kamati ya mazingira na masuala ya jamii ya Mabunge ya Afrika, Carribian na Pacific (ACP) kinachoendelea kufanyika huko Brussels Ubelgiji.
Katika taarifa yake Mh.Ndugai amezungumzia ongezeko kubwa la watu Duniani pamoja na ukosefu wa rasilimali za kuwahudumia.
Picha na Said Yakub

WACHIMBA MADINI NA WAVUVI HARAMU WASABABISHA MAPIGANO MOROGORO

Mkuu wa kituo cha polisi cha kati Morogoro ,Mkuu wa Upelelezi Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA wakiwa eneo la tukio bwawani Mindu
 Katika hali isiyokuwa ya kawaida wavuvi na wachimba madini haramu katika bwawa la Mindu walizua tafrani jana jioni baada ya wachimba madini watatu Andrea Michael, Juma Hassani na Yusuph Abdallah kukamatwa na Maaskari wa kampuni ya Mputa Security wanaolinda bwawa hilo.
Wachimba madini haramu waliokamatwa Mindu kutoka kulia Yusuph Abdallah,Juma Hassan na Andrea Michael
 Askari mmoja alipigwa na wavuvi baada ya kwenda kuwaondoa katika eneo lisiloruhusiwa kuvuliwa samaki, katika kujitetea wavuvi hao waliwapigia simu wenzao ambao walikuja na mapikipiki yapatayo 6 na kila pikipiki ikipakiza watu watatu watatu.
 Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA ilimbidi aende polisi kuchukua maaskari ili kuweza kuimarisha usalama katika bwawa hilo na wakati maaskari wanafika eneo la tukio wavamizi hao walikuwa wameshakimbia lakini walifanikiwa kupata mchimba madini mmoja aitwaye Juma Hassani na kwendanaye kituoni.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita akiongelea swala la kuzima mitambo ya maji na kusababisha mji karibu mzima kukosa maji alisema wamefikia hatua hiyo baada ya maji yaliyokuwa yakiingia kituo cha kutibia maji kuwa machafu sana na yananuka kutokana na mvua kuingiza maji machafu bwawani Mindu.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA akiongea na Chief Kingalu katika eneo la Mindu.

Waandishi wa habari wakiwahoji wachimba madini haramu waliokamatwa bwawani Mindu.


Wednesday, March 20, 2013

MVUA ZASABABISHA MITAMBO YA KUSAFISHA NA KUTIBIA MAJI KUZIMWA MOROGORO

Maji yakiwa yanamwagwa eneo la kutibia maji Mafiga.
 Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha wataalam katika kituo cha kutibu na kusafisha maji Mfiga iliyochini ya Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) kuzima mitambo na kumwaga maji yaliyokuwa yanaingia mitamboni hapo kutoka katika bwawa la Mindu kutokana na maji hayo kuwa machafu sana kwa kujaa tope.
Sampuli ya maji yaliyokuwa yanatoka bwawa la Mindu na kuja sehemu ya kutibia maji Mafiga.
 Hali hii ilizidi zaidi kutokana na mvua iliyonyesha jana jioni hadi usiku iliyoingiza tope jingi sana kwenye mdomo wa bomba la kuchukulia maji katika bwawa la Mindu.Hata hivyo wataalamu hao wamesema watawasha mitambo tu mara hali ya maji itakaporejea katika hali yake ya kawaida.
Kuzimwa kwa mitambo hiyo kumeathiri wakazi wa Maorogoro wanaotegemea chanzo cha Mindu kukosa maji ambao ni zaidi ya 70%.
Bi.Getrude Salema Afisa Uhusiano wa MORUWASA.
 Akiongea na Blogu hii Afisa Uhusiano wa MORUWASA Bi. Getrude Salema amesema hali hii ni changamoto kwa MORUWASA. Hata hivyo amewasihi wakazi wa Morogoro kuwa wawe wavumilivu na kuwa maji yatakayowafikia yatakuwa salama pale tu watakapokuwa wamewasha hiyo mitambo na kuruhusu maji yaanze kuingia na kutibiwa.
Mkondo wa maji ya mvua unaongiza tope bwawa la Mindu.
Blogu hii imefanya ziara hadi Mitambo ya kutibia maji Mafiga, Bwawa la Mindu na Sehemu ambako maji ya mvua yanavuka barabara ya Iringa na kuingia bwawa la Mindu.Kilichoonekana ni uchimbaji wa madini karibu na bwawa,mifugo kutifua ardhi pamoja na kilimo ndo sababu zilizochangia tope kuwa jingi.
Maji ya mvua yakiwa yametuama kando kando ya barabara ya Iringa eneo la Mindu
Hata hivyo,kando kando ya barabara ya Iringa kumeonekana madimbwi mengi ya maji yakiwa yametuama kutokana na makaravati yanayopitisha maji ya mvua kuziba kiasi cha kusababisha maji kukaa kwa muda mrefu na mvua zinaponyesha zinasomba hayo maji hadi bwawa la Mindu.

Wafanyakazi wa MORUWASA wakiwa wameenda kujionea halihalisi ya mikondo inayoingiza maji ya  mvua bwawani.

SAMAKI WA MAJITAKA WAHISIWA KUUZWA KWA WATU MJINI MOROGORO


Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, nikwamba vijana wenyeji wa Manispaa ya Morogoro wamekutwa wakikusanya samaki aina ya kambale katika mabwawa ya majitaka yanayotolewa tope ya Mafisa.
 Walipoulizwa wakasema wanaenda kula lakini uwalakini unakuja pale walipoonekana kukazana kukusanya samaki wengi na kwenda kuwasafisha.
 Wito wangu kwa wakazi wa Morogoro kuweni makini na samaki wanaouziwa na watu mitaani na kwa wale wenye mabucha kuweni waaminifu kwa kutonunua samaki watakao letwa kwao na vijana wa mtaani.
Na maafisa afya kuweni makini kwa kukagua samaki wanaouzwa kwenye mabucha na mitaani.

Monday, March 18, 2013

WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA HARAMBEE MAGOMENI



WAZIRI MKUU Ndg.Mizengo Pinda ameongoza harambee ya papo kwa papo na kufanikiwa kukusanya sh. milioni 31.5 zikiwa ni ahadi na fedha taslimu kwa ajili ya ukarabati wa Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda la Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waumini wa Kanisa hilo Jumapili asubuhi, Machi 17, 2013 kabla ya kuendesha harambee hiyo, Waziri Mkuu aliusifu uongozi wa Kanisa Katoliki la Magomeni kwa kuamua kufanya upanuzi wa kanisa hilo ili liweze kuhudumia waumini wengi zaidi.
“Nia yao ni nzuri sana na wameona mbali mapema. Magomeni hii ya leo si ya wakati ule, na wala haitakuwa hivi katika miaka mingine 50 ijayo. Zamani usingeweza kuona hata ghorofa moja hapa Magomeni lakini sasa hivi maghorofa hayahesabiki,” alisema.
Aliwasisitiza waumini hao kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu hakuna sadaka ambayo ni ndogo. “Hakuna sadaka iliyo ndogo mbele ya Mungu, kikubwa ni dhamira tu. Kanisa ni letu na litajengwa na sisi waumini ili mradi kila mmoja wetu aseme Kansa hili nitalijenga,” alisisitiza.
Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini hao, Baba Paroko wa kanisa hilo, Padri Sixfrious Rwechungura alisema wameanza kazi ya ukarabati tangu Agosti 15, 2011 na kwamba hadi sasa wamekwishakusanya sh. milioni 350 iliyotokana na nguvu za waumini wenyewe bila msaada wa kutoka nje.
Alisema wanahitaji kiasi cha sh. milioni 300 ili kukamilisha kazi hiyo ambayo inapaswa kukamilika katika miaka miwili ijayo ili iendane na maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo.
Katika harambee hiyo, Waziri Mkuu na mkewe Mama Tunu Pinda waliahidi kuchangia sh. Milioni 10 na kutoa sh. Milioni mbili za kianzio. Pia aliendesha mnada wa mbuzi aliyenunuliwa kwa sh. 600,000/- na mkoba ulionunuliwa kwa sh. 150,000/-.
(mwisho)

Friday, March 15, 2013

RAIS KIKWETE AKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 250 KATIKA HARAMBEE YA KUJENGA KANISA MOROGORO

Rais Kikwete akiendesha harambee
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa katoliki la Kigurunyembe iliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013 akiongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.
Rais Kikwete akiwa na Askofu wa jimbo la Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude.

MICHEZO: TANZANIA YAPANDA NAFASI 8 KATIKA VIWANGO VYA FIFA

 
Timu ya taifa ya Tanzania imepanda kiwango kwa nafasi 8 na katika viwango vya Afrika imepanda kwa nafasi 33.Kwa sasa Tanzania ni ya 119 huku Hispania ikibakia kuwa ya kwanza kwa ubora Duniani.
Kupanda kwa Tanzania kumetokana na kufanya vizuri kwenye michezo yake ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA.


Breaking news:WAHAMIAJI HARAMU 32 WAKAMATWA MKOANI RUKWA

Taarifa zilizotufikia hivi punde nikwamba Idara ya Uhamiaji mkoani Rukwa inawashikilia watu 32 wanao tuhumiwa kuwa wahamiaji haramu walioingia nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu katika maeneo tofauti ya nchi hii.
Taarifa zaidi tutawalete kadiri tutakavyokuwa tunazipata.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...