Wednesday, March 20, 2013
SAMAKI WA MAJITAKA WAHISIWA KUUZWA KWA WATU MJINI MOROGORO
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, nikwamba vijana wenyeji wa Manispaa ya Morogoro wamekutwa wakikusanya samaki aina ya kambale katika mabwawa ya majitaka yanayotolewa tope ya Mafisa.
Walipoulizwa wakasema wanaenda kula lakini uwalakini unakuja pale walipoonekana kukazana kukusanya samaki wengi na kwenda kuwasafisha.
Wito wangu kwa wakazi wa Morogoro kuweni makini na samaki wanaouziwa na watu mitaani na kwa wale wenye mabucha kuweni waaminifu kwa kutonunua samaki watakao letwa kwao na vijana wa mtaani.
Na maafisa afya kuweni makini kwa kukagua samaki wanaouzwa kwenye mabucha na mitaani.
Monday, March 18, 2013
WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA HARAMBEE MAGOMENI
Akizungumza
na waumini wa Kanisa hilo Jumapili asubuhi, Machi 17, 2013 kabla
ya kuendesha harambee hiyo, Waziri Mkuu aliusifu uongozi wa Kanisa
Katoliki la Magomeni kwa kuamua kufanya upanuzi wa kanisa hilo ili
liweze kuhudumia waumini wengi zaidi.
“Nia yao ni nzuri sana na wameona mbali mapema. Magomeni
hii ya leo si ya wakati ule, na wala haitakuwa hivi katika miaka
mingine 50 ijayo. Zamani usingeweza kuona hata ghorofa moja hapa
Magomeni lakini sasa hivi maghorofa hayahesabiki,” alisema.
Aliwasisitiza waumini hao kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu hakuna sadaka ambayo ni ndogo. “Hakuna
sadaka iliyo ndogo mbele ya Mungu, kikubwa ni dhamira tu. Kanisa ni
letu na litajengwa na sisi waumini ili mradi kila mmoja wetu aseme Kansa
hili nitalijenga,” alisisitiza.
Mapema
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini hao, Baba Paroko wa
kanisa hilo, Padri Sixfrious Rwechungura alisema wameanza kazi ya
ukarabati tangu Agosti 15, 2011 na kwamba hadi sasa wamekwishakusanya
sh. milioni 350 iliyotokana na nguvu za waumini wenyewe bila msaada wa
kutoka nje.
Alisema
wanahitaji kiasi cha sh. milioni 300 ili kukamilisha kazi hiyo ambayo
inapaswa kukamilika katika miaka miwili ijayo ili iendane na maadhimisho
ya miaka 50 ya kanisa hilo.
Katika
harambee hiyo, Waziri Mkuu na mkewe Mama Tunu Pinda waliahidi kuchangia
sh. Milioni 10 na kutoa sh. Milioni mbili za kianzio. Pia aliendesha
mnada wa mbuzi aliyenunuliwa kwa sh. 600,000/- na mkoba ulionunuliwa kwa
sh. 150,000/-.
(mwisho)
Friday, March 15, 2013
RAIS KIKWETE AKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 250 KATIKA HARAMBEE YA KUJENGA KANISA MOROGORO
Rais Kikwete akiendesha harambee |
Rais Kikwete akiwa na Askofu wa jimbo la Morogoro Mhashamu Telesphor Mkude. |
MICHEZO: TANZANIA YAPANDA NAFASI 8 KATIKA VIWANGO VYA FIFA
Timu ya taifa ya Tanzania imepanda kiwango kwa nafasi 8 na katika viwango vya Afrika imepanda kwa nafasi 33.Kwa sasa Tanzania ni ya 119 huku Hispania ikibakia kuwa ya kwanza kwa ubora Duniani.
Kupanda kwa Tanzania kumetokana na kufanya vizuri kwenye michezo yake ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA.
Kupanda kwa Tanzania kumetokana na kufanya vizuri kwenye michezo yake ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA.
Breaking news:WAHAMIAJI HARAMU 32 WAKAMATWA MKOANI RUKWA
Taarifa zilizotufikia hivi punde nikwamba Idara ya Uhamiaji mkoani Rukwa inawashikilia
watu 32 wanao tuhumiwa kuwa wahamiaji haramu walioingia nchini kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu katika maeneo tofauti ya nchi hii.
Taarifa zaidi tutawalete kadiri tutakavyokuwa tunazipata.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu katika maeneo tofauti ya nchi hii.
Taarifa zaidi tutawalete kadiri tutakavyokuwa tunazipata.
UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI KANDO MWA MTO RUVU
Wakazi wa kijiji cha Kibangile, Morogoro vijijini wakiwa wanaendelea na uchimbaji haramu wa madini. |
Uchimbaji madini kando mwa mto Ruvu |
Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu imekuwa na juhudi mbali mbali katika kuhakikisha uchimbaji haramu wa madini hauendelei katika kingo za mito ili kuifanya rasilimali maji inakuwa endelevu.
Uharibifu wa kingo za mto |
Thursday, March 14, 2013
RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA WAISLAM CHA MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi ametembelea Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM)
Jengo la ITC la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro lililowekwa jiwe la msingi na Rais Kikwete. |
Ziara ya Rais hii leo itaendelea kwa kuelekea Magadu Mesi ambako atafanya halambee ya kuchangisha fedha za kujenga kanisa katoliki la Kigurunyembe.
PAPA MPYA APATIKANA HUKO VATICAN
Papa Jorge Mario Bergoglio akisalimiana na Papa aliyejiuzulu. |
Hatimaye ile kazi ya kumchagua papa mrithi wa Papa Benedict XVI aliyejiuzulu mwezi Februari imekamilika baada ya Kadinali Jorge Mario Bergoglio kuchaguliwa na anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa
Papa na mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka kwenye dohani
katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku
ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne
kwa siku.
Maelfu ya watu kutoka
sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa
Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali
Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea
ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa
Monday, March 11, 2013
BALOZI WA IRELAND ATEMBELEA MIRADI YA MAJI MOROGORO
Balozi wa Ireland akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John.K.Mtaita. |
Balozi wa Ireland leo asubuhi ametembelea miradi ya maji mjini Morogoro inayofadhiliwa na Millenium Challenge Account-Tanzania (MCA-T). Katika ziara hiyo Balozi huyo ametembelea chanzo cha maji cha Mambogo ambako kunaukarabati mkubwa unaoendelea chini ya mradi huo kwa kujenga makingio ya maji, sehemu ya kutibia maji na birika la kusambazia maji.
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza kwa kiasi kikubwa adha ya upungufu wa maji iliyokuwa inawakabili wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa muda mrefu sasa kutokana na uchakavu wa miundombinu ya maji.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg.Joel.N.Bendera akisaini kitabu cha wageni |
Pamoja na kutembelea miradi hiyo pia balozi huyo ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).
Balozi wa Ireland akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalam Mshauri Ndg.Tom Killilea |
Balozi akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg.Joel.N.Bendera |
Friday, March 8, 2013
KIKAO CHA BODI YA MAJI CHAFANYIKA MOROGORO
Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Ndg.Washington Mutayoba na kulia ni Katibu wa Bodi Bi.Plaxeda Kalugendo |
Baadhi ya wajumbe la Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu wakisikiliza kwa makini. |
Rasilimali Maji katika Wizara ya Maji inasimamiwa na Ofisi za mabonde yapatayo tisa (9) katika nchi nzima.
Subscribe to:
Posts (Atom)