Monday, May 5, 2014

MKE WA RAIS NIGERIA ATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WA MAANDAMANO.

Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi habari zinasema.

Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Inasemekana Mke wa Rais Jonathan anahisi mama za wasichana waliotekwa walimtuma mwanaharakati huyo ili aweze kuwawakilisha.
Mchambuzi wa masuala ya Nigeria anasema Mke wa Rais Jonathan ni Mwanasiasa mwenye nguvu nchini Nigeria.
Mama Mutah mwakilishi wa jamii ya Chibok eneo wasichana hao walipotekwa wakiwa shuleni zaidi wiki mbili zilizopita, wiki iliyopita aliandaa maandamano katika mji mkuu wa Abuja.
Waandamanaji wengi wakiwa ni Wanaigeria wanaona serikali haijafanya vya kutosha kuwatafuta wasichana hao waliotekwa wanaodhaniwa kuwa ni kundi la kiislam la Boko Haram.

Hadi sasa Boko haram hawajasema lolote kuhusu tuhuma hizo.
Wasichana wanne walio mbele ambao ni miongoni mwa waliotekwa na kufanikiwa kutoroka.


Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...