Tuesday, April 14, 2015

Al Shabaab waua watu 9 katika majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.

Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo

kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab,
amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa
''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu''
Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.
Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo.
hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo .
Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...