Wednesday, April 16, 2014

Updates: WALIONUSURIKA KATIKA MELI ILIYOZAMA KOREA WASIMULIA.

Meli ya Korea Kusini ikizama
Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha."watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...