Monday, February 11, 2013
BREAKING NEWS: MAPIGANO YA KIDINI YAPOTEZA MAISHA YA RAIA BUSELESELE GEITA
Tuesday, February 5, 2013
KITALE AFUNGA NDOA NA KUUAGA UKAPELA.
Kitale akiwa na mkewe Bi Fatuma |
Hatimaye msanii wa filamu za komedi ameamua kuuaga ukapela na kuoa baada ya hiyo jana kufunga pingu za maisha na mke wake Bi Fatuma Salumu.
Kitale akiwa anafungishwa nikhai |
Ndoa hiyo ilifungiwa maeneo ya Mwananayamala jijini Dar es salaam mnamo saa nane hivi mchana.Kama kazi yake inavyohakisi,sherehe za ufungaji wa ndoa hiyo ziliudhuriwa na watu wengi ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa.
Monday, February 4, 2013
BREAKING NEWS: MOTO WAIBUKA NA KUUNGUZA VITU STENDI YA MWENGE
Friday, February 1, 2013
BREAKING NEWS: MVUA ZALETA MAAFA MJINI MOROGORO
Barabara Morogoro ikiwa imejaa maji |
Mvua zinazoendelea kunyesha mjini Morogoro zinazidi kuleta maafa baada mvua zilizonyesh usiku wa leo zimewaathiri wakazi wa hapa baada ya nyumba kujaa maji na baadhi ya barabara kufungwa kutokana na kujaa maji.
Maji yakiwa yamejaa barabarani eneo la Mtawala karibu na uwanja wa Shujaa |
Magari yakiwa yanajiuliza namna ya kupita katika barabara Uwanja wa Shujaa. |
Tatizo hili limeweza kuzikumba na baadhi ya Ofisi za Serikali ambapo katika ofisi za MORUWASA na Ofisi za Bonde la Wami/Ruvu maji yalijaa getini kiasi cha wafanyakazi wenye magari kushindwa kupita na kusubiri maji yapungue.
Geti la ofisi za MORUWASA na Bonde la Wami/Ruvu likiwa limejaa maji. |
Thursday, January 31, 2013
HABARI ZILIZOVUNJIKAVUNJIKA:JAHAZI SUNRISE YAZAMA NUNGWI ZNZ
Jahazi SUNRISE ambayo ilikuwa
ikitokea Mkoani Tanga kulekea visiwani Zanzibar ikiwa na abiria 32
imezama eneo la Nungwi huku jitihada za kuwaokoa abiria hao zikiendelea
kufanywa na maofisa wa uokoaji mpaka sasa.
Kwa habari zaidi fuatilia hapa hapa.
KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOIVAA CAMEROON CHATAJWA,MAFTAH NA TEGETE WATOSWA.
![]() |
Tegete kushoto akiwa na Kiiza |
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21
kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya
mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim
amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu
ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa
mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili
yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco.
Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka
kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza
fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya
mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea
nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory
Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la
Dunia.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco,
Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi
ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu
nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji
aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini
Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam),
Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa
Sugar).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam),
Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho
Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI NA MAASKARI WENZAKE WAMCHEFUA HAKIMU.
![]() |
Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi akiwa katika viwanja vya Mahakama |
Askari
waliomleta mahakamani mtuhumiwa askari wa FFU mwenye namba G2573
Pasificus Cleophace Simoni (23) wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa
habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi,
wamemtibua Hakimu aliyeagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani
hapo kwa kudharau mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa mnyeti wetu kutoka mahakamani hapo,tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 5.35 asubuhi mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo. Askari watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .
Mahakama ikiwa bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.
Wakati hakimu huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria wa Mahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa mnyeti wetu kutoka mahakamani hapo,tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 5.35 asubuhi mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo. Askari watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .
Mahakama ikiwa bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.
Wakati hakimu huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria wa Mahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa bila utaratibu wa mahakama hebu mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona wanafanya fujo mahakamani hao.Pamoja na jitihada za mwanasheria wa serikali Adolf Maganda kuwaita kwa sauti, askari hao kuwataka kumrudisha ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo bali walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda naye mahabusu.
Baada ya dakika kama 5 hivi, ndipo mwanasheria huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambaye hata hivyo hakwenda kusimama kizimbani na badala yake alikwenda upande wa kushoto wa mahakama ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama kuanza na kuketi katika kiti huku akiwa bado amevaa miwani na kofia yake.
Kutokana na tukio hilo, Hakimu huyo alilazimika kuwahoji askari hao watatu kwa vurugu hizo walizozifanya kwa kuwauliza swali moja pekee , ikiwa wanaona walichofanya ni sahihi, ambapo askari hao waliosema, “samahani mheshimiwa”.
Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Adolf Maganda aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ambayo awali ilikuwa imetajwa Januari 27, 2013 lakini mtuhumiwa alishindwa kufika Mahakamani kutokana na ugonjwa. Mahakama hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 mwaka huu.
![]() |
Jinsi marehemu Mwangosi alivyokuwa akikabiliwa na maaskari kabla ya umauti kumkuta. |
Wednesday, January 30, 2013
WATUMISHI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAPATA AJALI
![]() |
Gari la Wizara lililopinduka |
Watumishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wapata ajali kilometa ishirini kabla ya kufika mkoa wa Dodoma wilaya ya Bahi,ajali hiyo ilisababishwa na cheni ambayo ilitumika kuwavuta maafisa wengine waliokwama wakiwa safarini kuelekea mkoani Mara (Musoma) kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya MTUHA,hali za watumishi (Enock Mhehe,Shoo,Mtimbika na Muhasibu kutokea Singida) zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu Hospitali ya mkoa Dodoma na kurushusiwa kuendelea na safari.
![]() |
Magari yaliyopata ajali |
MVUA ZILIZONYESHA JANA MOROGORO
Bwawa la Mindu |
Jana kulinyesha mvua kubwa sana Mjini Morogoro kiasi cha kuwasababishia madhara baadhi ya wakazi wa Manispaa wanaoishi mabondeni ikiwa ni pamoja na kusombwa kwa baadhi ya nyumba.
Mkazi wa Morogoro akifurahi baada ya mvua kunyesha hiyo jana |
Lakini pamoja na kunyesha kwa mvua hizo hali ya maji katika bwawa la Mindu haikubadilika sana maana mpaka kufika leo saa 9.30 mchana maji yalikuwa yameongezeka kwa kiasi cha sentimeta sita (sm 6),lakini kiasi cha maji yanayoingia bwawani kinaweza kuwa kimebadilika na kuongezeka kufika kesho asubuhi maana mito inaendelea kuingiza maji bwawani.
TAIFA STARS KUKIPIGA NA CAMEROON
![]() |
Kikosi cha Taifa stars |
Timu ya taifa mpira wa miguu ya Tanzania Taifa stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Cameroon mchezo utakaopigwa Februari 06,2013 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 11 kamili jioni.
Kikosi cha Cameroon kinatarajiwa kuwasili hapa nchini tarehe 03 Februari,2013 kwaajiri ya mtanange huo.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo upo katika calenda ya FIFA,hivyo matokeo ya mchezo huo yanatumika kutuweka kwenye nafasi za viwango vya FIFA.
Subscribe to:
Posts (Atom)