Tuesday, February 5, 2013

KITALE AFUNGA NDOA NA KUUAGA UKAPELA.

Kitale akiwa na mkewe Bi Fatuma
 Hatimaye msanii wa filamu za komedi ameamua kuuaga ukapela na kuoa baada ya hiyo jana kufunga pingu za maisha na mke wake Bi Fatuma Salumu.
Kitale akiwa anafungishwa nikhai
 Ndoa hiyo ilifungiwa maeneo ya Mwananayamala jijini Dar es salaam mnamo saa nane hivi mchana.Kama kazi yake inavyohakisi,sherehe za ufungaji wa ndoa hiyo ziliudhuriwa na watu wengi ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa.


Monday, February 4, 2013

BREAKING NEWS: MOTO WAIBUKA NA KUUNGUZA VITU STENDI YA MWENGE

Moto uliozuka katika maduka ya eneo la Mwenge kituo cha mabasi umedhibitiwa na vikosi vya zimamoto na sasa hali ni shwari ingawa shughuli nyingi za kibiashara bado zimesimama wahusika wakihofia usalama wa mali zao.

Friday, February 1, 2013

BREAKING NEWS: MVUA ZALETA MAAFA MJINI MOROGORO

Barabara Morogoro ikiwa imejaa maji

Mvua zinazoendelea kunyesha mjini Morogoro zinazidi kuleta maafa baada mvua zilizonyesh usiku wa leo zimewaathiri wakazi wa hapa baada ya nyumba kujaa maji na baadhi ya barabara kufungwa kutokana na kujaa maji.
Maji yakiwa yamejaa barabarani eneo la Mtawala karibu na uwanja wa Shujaa


Magari yakiwa yanajiuliza namna ya kupita katika barabara Uwanja wa Shujaa.

Tatizo hili limeweza kuzikumba na baadhi ya Ofisi za Serikali ambapo katika ofisi za MORUWASA na Ofisi za Bonde la Wami/Ruvu maji yalijaa getini kiasi cha wafanyakazi wenye magari kushindwa kupita na kusubiri maji yapungue.

Geti la ofisi za MORUWASA na Bonde la Wami/Ruvu likiwa limejaa maji.


Thursday, January 31, 2013

HABARI ZILIZOVUNJIKAVUNJIKA:JAHAZI SUNRISE YAZAMA NUNGWI ZNZ

Jahazi SUNRISE ambayo ilikuwa ikitokea Mkoani Tanga kulekea visiwani Zanzibar ikiwa na abiria 32 imezama eneo la Nungwi huku jitihada za kuwaokoa abiria hao zikiendelea kufanywa na maofisa wa uokoaji mpaka sasa.
Kwa habari zaidi fuatilia hapa hapa.

KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOIVAA CAMEROON CHATAJWA,MAFTAH NA TEGETE WATOSWA.


Tegete kushoto akiwa na Kiiza

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI NA MAASKARI WENZAKE WAMCHEFUA HAKIMU.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi akiwa katika viwanja vya Mahakama

Askari waliomleta mahakamani mtuhumiwa askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)  wa mauwaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi,   wamemtibua Hakimu aliyeagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani hapo kwa kudharau mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa mnyeti wetu kutoka mahakamani hapo,tukio  hilo lilitokea leo  majira ya saa 5.35 asubuhi mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo. Askari  watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa  kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .

Mahakama ikiwa  bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi  wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani  huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza  kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.

Wakati hakimu  huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku  hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria  wa Mahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha  na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa  bila utaratibu wa mahakama hebu  mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona  wanafanya fujo mahakamani  hao.
Pamoja na jitihada za mwanasheria wa  serikali Adolf Maganda kuwaita  kwa  sauti,  askari hao  kuwataka  kumrudisha  ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo  bali  walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda naye mahabusu. 

Baada ya dakika kama 5 hivi, ndipo mwanasheria  huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambaye hata  hivyo hakwenda kusimama  kizimbani na badala  yake alikwenda upande wa  kushoto wa mahakama ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama  kuanza na kuketi katika  kiti huku akiwa bado amevaa miwani na kofia  yake.

Kutokana na  tukio  hilo, Hakimu  huyo alilazimika  kuwahoji askari hao  watatu kwa vurugu  hizo  walizozifanya kwa kuwauliza swali moja  pekee , ikiwa wanaona walichofanya ni  sahihi, ambapo askari hao waliosema, “samahani mheshimiwa”.

Mwendesha mashtaka  wa Jamhuri, Adolf Maganda aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena  kwa kesi hiyo ambayo awali ilikuwa imetajwa Januari 27, 2013 lakini mtuhumiwa alishindwa kufika Mahakamani kutokana na ugonjwa. Mahakama  hiyo  imeahirisha  kesi hiyo  hadi  Februari 14 mwaka huu.

Jinsi marehemu Mwangosi alivyokuwa akikabiliwa na maaskari kabla ya umauti kumkuta.
Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa  bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Ten  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  zilipozuka vurugu kati ya  Askari Polisi na wafuasi wa  CHADEMA.

Wednesday, January 30, 2013

WATUMISHI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAPATA AJALI

Gari la Wizara lililopinduka

Watumishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wapata ajali kilometa ishirini kabla ya kufika mkoa wa Dodoma wilaya ya Bahi,ajali hiyo ilisababishwa na cheni ambayo ilitumika kuwavuta maafisa wengine waliokwama wakiwa safarini kuelekea mkoani Mara (Musoma) kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya MTUHA,hali za watumishi (Enock Mhehe,Shoo,Mtimbika na Muhasibu kutokea Singida) zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu Hospitali ya mkoa Dodoma na kurushusiwa kuendelea na safari.

Magari yaliyopata ajali

MVUA ZILIZONYESHA JANA MOROGORO


Bwawa la Mindu

Jana kulinyesha mvua kubwa sana Mjini Morogoro kiasi cha kuwasababishia madhara baadhi ya wakazi wa Manispaa wanaoishi mabondeni ikiwa ni pamoja na kusombwa kwa baadhi ya nyumba.
Mkazi wa Morogoro akifurahi baada ya mvua kunyesha hiyo jana
Lakini pamoja na kunyesha kwa mvua hizo hali ya maji katika  bwawa la Mindu haikubadilika sana maana mpaka kufika leo saa 9.30 mchana maji yalikuwa yameongezeka kwa kiasi cha sentimeta sita (sm 6),lakini kiasi cha maji yanayoingia bwawani kinaweza kuwa kimebadilika na kuongezeka kufika kesho asubuhi maana mito inaendelea kuingiza maji bwawani.

TAIFA STARS KUKIPIGA NA CAMEROON

Kikosi cha Taifa stars

Timu ya taifa mpira wa miguu ya Tanzania Taifa stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Cameroon mchezo utakaopigwa Februari 06,2013 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 11 kamili jioni.
Kikosi cha Cameroon kinatarajiwa kuwasili hapa nchini tarehe 03 Februari,2013 kwaajiri ya mtanange huo.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo upo katika calenda ya FIFA,hivyo matokeo ya mchezo huo yanatumika kutuweka kwenye nafasi za viwango vya FIFA.

UKAME MKALI WAIKUMBA MOROGORO

Bwawa la Mindu likiwa limekauka kwa ukame

Hali ya mji wa Morogoro inazidi kuwa mbaya baada ya kutonyesha mvua kwa muda mrefu.Ukame huu umepelekea maji katika bwawa la maji la Mindu kukauka na kupungua kina cha maji kwa meta 2 (2m)
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mjisafi na Usafi wa mazingira Morogoro wamefanya ziara ya kutembelea vyanzo vya maji na kujionea upungufu wa maji .
Wajumbe wa Balaza la Wakurugenzi wa MORUWASA pamoja na watendaji wakiwa wanaangalia jinsi bwawa lilivyokauka.

Katika kujumuisha ziara hiyo,Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa amewasihi wananchi wote pamoja na wanasiasa kushirikiana katika suala zima la utunzaji wa mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MORUWASA Bibi Dynes Senyagwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita amesema suala hili la uharibifu wa Mazingira linasababisha "mgao wa maji ndani ya mgao" kutokana na upungufu huo wa maji.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John K.Mtaita







LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...