Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Thursday, July 4, 2013

RAIS MPYA WA MISRI KUAPISHWA LEO.

Sherehe za baada ya kumuondoa mamlakani Morsi.
Jaji mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Misri Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumng'oa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.

Chanzo: BBC

RAIS MOHAMED MORSI WA MISRI APINDULIWA.

Jeshi la Misri limesitisha Katiba ya nchi hiyo na kumvua madaraka Rais Mohamed Morsi na kutangaza kuwa Jaji mkuu atashika hatamu za uongozi kwa sasa.
Baada ya mapinduzi hayo kufanyika,vyombo vya usalama vimemweka kizuizini Mohamedi Morsi.

Katika hatua nyingine kufuatia mapinduzi hayo,Rais Ballack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wametaka utawala wa kiraia kurejeshwa haraka nchini humo.
Waasi wa Morsi wakishangilia baada ya Jeshi kutangaza kuondolewa kwa Rais madarakani.
Kwa habari zaidi juu ya mapinduzi hayo, endelea kutembelea blogu hii.

Monday, July 1, 2013

Rais wa zamani wa Chad akamatwa Senegal.

Polisi nchini Senegal , wamemkamata rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre, aliyekuwa anatafutwa kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wake wa miaka 8.
Wakili wa Bwana Habre, El Hadji Diouf, alisema kuwa alikamatwa na polisi kutoka nyumbani kwake mjini Dakar na kupelekwa sehemu isiyojulikana.
Habre mwenye umri wa miaka 70, amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani, nchini Senegal tangu mwaka 2005 alikokimbilia baada ya kung'olewa mamlakani mwaka 1990.
Aanatuhumiwa kuwatesa maelfu ya watu, wanaominika kuwa wapinzani wake.
Mwaka jana mahakama ya kimataifa ya haki, iliamuru Seengal kumchukuliwa hatua za kisheria au kupeleka kwingineko ambako atakabiliwa na sheria kwa uhalifu aliotenda.
Kukamatwa kwake kunakuja siku kadhaa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumsifu rais Macky Sall kwa hatua zake za kuelekea katika kumfungulia mashtaka Habre mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamekuwa yakishinikiza Senegal kwa miaka mingi, kumfungulia mashtaka Habre.
Tuhuma anazokabiliwa nazo ni za tangu mwaka 1982, wakati alipoingia mamlakani hadi mwaka 1990 alipoondolewa uongozini kwa njia ya mageuzi .
Habre alishtakiwa kwa mara ya kwanza nchini Senegal mwaka 2000, lakini mahakama za nchi hiyo ikaamua kuwa wakati huo isingeweza kushtakiwa huko.
Waathiriwa wa utawala wake baadaye waliwasilisha malalamishi chini ya sheria ya kimataifa ya Ubelgiji ambayo inaruhusu majaji wake kusikiliza na kuhukumu washukiwa wa kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu kokote duniani.
Hata hivyo Senegal imekataa ombi la Ubelgiji kumhamisha nchini humo ili ahukumiwe.

Chanzo:BBC

MISRI HALI TETE,RAIS ATAKIWA KUJIUZULU HADI KUFIKiA KESHO.

Umoja wa vyama vya upinzani unaompinga Rais Mohammed Morsi wa Misri, umemtaka Rais huyo kujiuzulu hadi kufikia kesho au atarajie uasi zaidi,na hii ikiwa ni mwaka mmoja tangu aingie madarakani. Siku ya jana ilimalizika kwa kuwashuhudia watu wakimiminika mitaani kwenye mji mkuu, Cairo. Wapinzani wanalituhumu kundi la Udugu wa Kiislamu la Rais Morsi kwa kuyateka mapinduzi ya umma, kupitia ushindi kwenye uchaguzi, kujilimbikizia madaraka na kutaka kuweka Sharia ya Kiislamu. Waandamanaji wengine wanasema wamevunjwa moyo na mgogoro wa kiuchumi. Maafisa wa usalama wanasema ofisi tatu za chama cha Udugu wa Kiislamu zilichomwa moto na waandamanaji kwenye jimbo la Nile Delta. Zaidi ya wafuasi 20,000 wa Rais Morsi pia walikusanyika karibu na kasri ya Rais mjini Cairo kumuunga mkono kiongozi huyo.

Thursday, June 27, 2013

WAFANYABIASHARA WAGOMA UGANDA KWA SIKU 3 SASA.

Maduka yamesalia kufungwa mjini Kampala Ugana kwa siku ya tatu leo huku wafnyabiashara wakigoma kuhusiana na mpango wa serikali kusisitiza viwango vya biadhaa zinazoingizwa nchini humo kuwa za juu.

Chama cha wafanyabiashara hao kinasema kinapinga gharama wanayotozwa ikiwa bidhaa wanazoingiza nchini humo sio za viwango vya juu. Malipo hayo ni kodi iliyoanza kutozwa na serikali hivi karibuni ambayo inagharamia kuchunguzwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo
Wanatak serikali ikome kuwatoza ushuru huo kwani wafnyabiashara tayari wanatozwa kodi ya juu.
Duru zinasema kuwa vuguvugu la upinzani linatarajiwa kujiunga na maandamano hayo, na kuwa polisi wamedhibiti hali ya usalama mjini Kampala.
Mwandishi wa BBC mjini humo Catherine Byaruhanga anasema kuwa polisi huenda wakavunja maandamano hayo kwa kuhofia otovu wa usalama.
Waziri wa biashara, Amelia Kyambadde, ameelezea wazi kuwa Uganda inashinikizwa na wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa iweze kutekeleza vikwazo vya kuhakikisha kuwa bidhaa zinzoingizwa nchini humo ziwe za hali ya juu.
Kodi hiyo inalenga kuondoa uwezekano wa wafanyabiashara kuingiza biadhaa ghushi nchi humo swala ambalo Uganda inatuhumiwa kutokuwa maakini nalo katika kulitokomeza.
Wafanyabiashara wanapaswa kuingiza nchini humo bidhaa za hali ya juu kutoka kwa watengezaji wanaojulikana na ambao wako kwenye orodha inayojulikana kwa mataifa ya Afrika Mashariki, ingawa wanasema kuwa gharama inayopaswa kulipwa kwa hilo kufanyika ni ya juu zaidi.

Source:BBC

JACOB ZUMA AHAIRISHA SAFARI YA MSUMBIJI BAADA YA HALI YA MANDELA KUZIDI KUZOROTA.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.
Mandela ambaye, ni Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.

Tuesday, June 25, 2013

NELSON MANDELA TAABANI.

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Afrika Kusini zinasema Afya ya Nelson Mandela yazidi kuzorota .Familia yake yakusanyika Hospitali pretoria na kufanya kikao cha dharura kujiandaa kwa lolote litakalojiri.

WATU 4 WAMENYONGWA NIGERIA.


Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba.
Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji.




Shirika la Amnesty International lilisema kuwa hatua hiyo ya kuwanyonga wafungwa ni jambo la kuhuzunisha sana kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Nigeria.

Zaidi ya wafungwa 1,000 nchini Nigeria wanaaminika kuhukumiwa kifo .
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Rais Goodluck Jonathan hivi karibuni aliwataka magavana wa majimbo kutia saini vibali vya hukumu ya kifo katika jitihada za serikali kupunguza visa vya uhalifu.
Bwana Idahagbon alisema kuwa wananume wanne walinyongwa katika gereza la Benin baada ya mahakama kuamuru wanyongwe siku ya Jumatatu.
Alisema kesi zote za rufaa, hazikuweza kufua dafu na hukumu zao tayari zikuwa zimetiwa saini -mbili na magavana wa Edo Governor Adams Oshiomhole, huku nyingine zikitiwa saini na magavana wa majimbo mengine.
Ikiwa itathibitishwa , hatua hii ya kunyongwa ni ishara ya kurejea kwa sheria kali ya hukumu ya kunyongwa nchini Nigeria.
Wahudumu wa magereza ndio waliotekeleza hukumu ya kunyongwa , kitengo cha serikali wala sio jimbo la Edo.
Kulikuwa na ripoti za kutatanisha kuhusu hali ya mfungwa wa tano.
Chino Obiagwu wa kitengo cha sheria na mradi wa kuwasaidia wafungwa hao alisema kuwa mwanaume huyo alinyongwa.
Hukumu ilicheleweshwa kwa muda kwa sababu za kiufundi lakini baadaye wakapashwa habari kwa njia ya barua pepe, alisema bwana Obiagwu.
Lakini bwana Idahagbon alisema mwanaume huyo hakunyongwa kwa sababu hukumu yake ilisema kuwa auawe kwa kupigwa risasi.
Hata hivyo shirika la Amnesty International limesema kuwa limepokea habari zinazoweza kuthibitisha kuwa wafungwa wanne walinyongwa mjini Benin.

source:BBC

Monday, June 24, 2013

Walimu watangaza mgomo rasmi Nchini Kenya.


Chama cha kitaifa cha walimu nchini Kenya, kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia leo baada ya serikali kukosa kuwalipa marupurupu yao.Huu ni mgomo wa saba wa walimu tangu mwaka 2007.

Mwnyekiti wa kitaifa wa chama hicho,Wilson Sossion alituhumu serikali kwa kucheza siasa na maswala yanayowahusu walimu kwani wanafahamau masaibu ya walimu na mkataba wa mwaka 1997 uliotoa ahadi ya marupurupu hayo kwa walimu.


Kulingana na makubaliano hayo, serikali inapaswa kuwalipa walimu marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu , kuwlaipia nyumba , matibabu na pesa za usafiri.
"tumedurusu mienendo ya serikali na kugundua kuwa wantumia mtindo wa kugawanya watu. Hilo halitafanya halitafaulu,'' alisema bwana Sossion
"Tumetangza kuwa mgomo wa waalimu unaanza rasmi leo, '' aliongeza bwana Sossion
Sossion pia alisema kuwa tume ya kushughulikia maswala ya walimu, haina mamlaka ya kuwaamuru walimu kutogoma au vinginevyo kwani hilo ni jukumu la Knut.
Katibu mkuu Knut, bwana Nyamu aliseama kuwa chama cha walimu kimeweka bayana matakwa yao waliyokubana na serikali mwaka 1997.
"marupurupu haya yote sharti yalipwe.Tumekwenda kwa wizara ya limu ya kuelezea malalmiko yetu,'' alisema bwana Nyamu.
"tunawaambia walimu kuwa katibu mkuu atawapa maagizo kuhusu watakachofanya wakati wa mgomo huu. Walimu waanze kwa kukabidhi majukumu yao katika shule zao leo.
Nyamu pia aliwataka walimu kuwaondoa watoto wao shuleni kwani walimu hawatakuwepo kuwafundisha.
''Kwa sasa tunaiacha serikali ifanye uamuzi , tutaketi chini na kusubiri,'' alisema Nyamu
''Wanachokitaka walimu ni pesa, na wale wanaomshauri rais wamwambie kuwa lazima walimi wapewe pesa kwani hawatazungumzia kingine ila marupurupu yao,'' alisema Sossion

Source: BBC

WATU 10 WAMEUAWA HOTELINI- PAKISTAN.


Watu 10 wameuawa katika hoteli,kaskazini mwa   Pakistan ikiwa pamoja na watalii tisa .
Watu waliokuwa na silaha waliivamia kambi moja ya  sehemu hiyo ya Nanga Parbat na kuwaua  watalii hao.
Kwa mujibu wa taarifa, waliouawa walikuwa raia wa Ukraine,Urusi na China.
Msaidizi wa watalii,mwenyeji wa sehemu hiyo pia aliuawa.
Marekani pia imethibitisha kwamba raia wake mmoja alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Washambuliaji 15 waliojifanya kuwa ni polisi waliivamia kambi hiyo katika jimbo la Gilgit-Baltistan
Kwa mujibu wa taarifa za mashirika ya habari, Taliban wamedai kuhusika na mashambulio hayo.
Msemaji wao ameeleza kuwa watu hao wameuliwa  kulipiza kisasi kifo cha makamu kiongozi wa Taliban ,Wali ur Rehman alieuliwa katika shambulio la  mwezi uliopita lililofanywa na ndege ya Marekani inayoruka bila ya rubani.

Source: DW

Friday, June 21, 2013

MAFURIKO YAUA WATU ZAIDI YA 300 INDIA.

Makundi ya waokoaji yanaendelea kuwatafuta walionusurika katika mafuriko yaliotokea katika jimbo la Uttarakhand nchini India leo, huku maafisa wakisema karibu watu 300 wamekufa.
Taarifa zinasema zaidi ya watu 13,800 wamepotea na wengine 62,800 wangali wamenasa katika maeneo hayo  karibu na miji ya shughuli za  hija za  waumini wa kihindu ya  Badrinath na Kedarth.
Picha za televisheni zimeonyesha watu wakipanda mabonde, huku wakisaidiwa na wanajseshi. Hadi sasa karibu watu 56,000 wameokolewa.

Source: DW

Wednesday, June 19, 2013

OFISI ZA UN ZASHAMBULIWA SOMALIA.


Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia makao ya umoja wa mataifa mjini Mogadishu Somalia .
Mlipuko mkubwa ulisikika ukifuatiwa na milio mikubwa ya risasi.

Duru zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga ndiye alijilipua katika lango kuu la makao hayo kisha watu waliokuwa wamejihami wakaingia ndani ya ofisi na kuanza kufyatua risasi.

Makao yenyewe yako karibu na uwanja wa ndege na yana nyumba za wafanyakazi wa umoja wa mataifa .
Wavamizi walishambulia ofisi za makao ya shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
Majeshi ya Somalia na yale ya Muungano wa Afrika, walizingira makao ya shirika hilo na kuanza kufyatua risasi kujaribu kuwatimua washambuliaji hao.
Kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Ofisi hizo ni makao kwa maafisa wa Umoja wa mataifa walio mjini Mogadishu.Hili ndilo shambulizi kubwa zaidi kushuhudiwa kwa siku za karibuni dhidi ya Umoja wa mataifa mjini Mogadishu.

Source:BBC

Thursday, June 13, 2013

WATOTO 93,000 WAMEUAWA SYRIA.

Makaburi ya watu waliouawa nchini Syria.
Umoja wa Mataifa umesema takriban watoto elfu tisini na tatu wameuawa nchini Syria tangu kuanza kwa mapigano nchini humo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo imeongezeka kwa zaidi ya elfu thelathini, tangu umoja huo ulipotoa takwimu zake Januari mwaka huu.
Ripoti hiyo imesema kuwa watu elfu tano hufa nchini Syria kila mwezi tangu Julai mwaka uliopita
Hata hivyo takwimu hizo huenda sio idadi kamili na Umoja wa Mataifa umesema huenda idadi ya waliouawa huenda ikawa kubwa zaidi, kwa kuwa vifo vingi havijaripotiwa.
Asilimia themanini ya waliouawa ni wanaume, lakini Umoja huo umeongeza kusema kuwa tayari umethibitisha kutokea kwa vifo vya zaidi ya watoto elfu moja mia saba ambao wako chini ya umri wa miaka kumi.
Vile vile, kuna ripoti kuwa watoto wengine waliteswa kabla ya kuuawa kinyama.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadam Navi Pilllay, amesema wamepokea ripoti ya kutokea kwa mauaji ya familia nyingi wakiwa na watoto wao, ishara kuwa vita vinavyoendelea nchini Syria vimegeuka kuwa janga kuu huku maelfu ya watu wakiendelea kuuawa kila siku.

Source: BBC.

Monday, June 10, 2013

WATU ZAIDI YA 15 WAJERUHIWA KENYA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI YA MAGURUNETI.

Takribani watu 15 wamejeruhiwa katika milipuko ya maguruneti nchini Kenya Jumapili usiku. Mashambulizi hayo yalifanywa mjini Mombasa mtaa wa Likoni na Nairobi katika mtaa wa Eastleigh yote chini ya kipindi cha masaa mawili.
Shambulizi la mjini Mombasa, lilifanyika katika kanisa moja saa moja usiku Jumapili na kuwajeruhi watu 12 wakati shambulizi la Niarobi lilitokea katika hoteli moja huku watu watatu wakijeruhiwa.




Waathiriwa mjini Nairobi walikimbizwa hospitalini kwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta kwa matibabu zaidi.

Maafisa wakuu mjini Mombasa walielezea kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokana na shambulizi hilo lakini kulikuwa na ripoti kuwa baadhi ya waathiriwa walilazwa katika hospitali kuu mjini Mombasa wakiwa hali mahututi.
Polisi walisema kuwa watu sita akiwemo mwanfunzi wa darasa la nne pamoja na mhubiri walijeruhiwa katika kile kilichosemekana kuwa shambulizi la guruneti katika kanisa la Earthquake Miracle Ministries.
Waathiriwa zaidi walijeruhiwa katika msongamano wa watu waliokuwa wanakimbilia usalama wao baada ya kuzuka kwa moto kufuatia gurunti hilo.
Matukio hayo ya usiku wa kuamkia leo, yanazua wasiwasi kuhusu kuibuka tena kwa mashambulizi ya kigaidi katika miji hiyo miwili baada ya miezi kadhaa ya kutokuwepo mashambulizi.
Duru zinasema kuwa shambulizi la Nairobi lilitokana na guruneti lililorushwa kutoka kwa gari iliyokuwa inakwenda kwa kasi, wakati shambulizi la mjini Mombasa lilitokea wakati mtu aliyekuwa anaendesha pikipiki aliporushia guruneti kikundi cha watu.
Duru zinasema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mashambulizi hayo.
Kufikia Jumapili, usiku, wataalamu walikuwa bado wanakusanya ushahidi mjini Mombasa kubaini nia ya mlipuko uliotokea na ikiwa lilikuwa shambulizi la guruneti au kifaa kilichotengezwa mfano wa bomu.
Mashambulizi kama haya yamekuwa yakishuhudiwa tangu jeshi la Kenya kujiunga na majeshi ya AU katia harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram.

Source:BBC

MKUU WA MAJESHI LIBYA AJIUZURU.

Mkuu wa majeshi nchini Libya Youseff al Man Gous amejiuzulu siku moja baada ya ghasia mashariki mwa mji wa Benghazi kusababisha vifo vya watu 31.Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumamosi wakati waandamanaji walipovamia kambi ya kundi la wanamgambo wanaojulikana Shield wanaoiunga mkono serikali.Kundi hilo pia ndilo lililo na jukumu la  kulinda amani katika eneo hilo la Benghazi.Waandamanaji hao walikuwa wanataka wanamgambo hao wakabidhi madaraka ya kiusalama kwa  kikosi rasmi cha usalama cha Libya na wasalimishe silaha zao. Bunge la kitaifa la Libya limetangaza kujiuzulu kwa Youseff  ambaye ameshutumiwa kwa kuchelewa kuunda jeshi la kitaifa na kutangaza pia siku tatu za maombolezi.

Source:DW

Thursday, May 30, 2013

URUSI YAIKABIDHI SYRIA 'ZANA ZA KIVITA'

Syria imepokea ngao za kwanza kutoka kwa Urusi, za kuikinga nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya makombora ya angani. Hii ni kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.
Urusi imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuhami Syria, mara tu baada ya uamuzi wa muungano wa Ulaya wa kuondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha.
Bwana Assad pia anaripotiwa kuambia televisheini yenye uhusiano na kundi la Hezbollah, kuwa sasa kumekucha kwani vita ndio vinaanza kushika kasi.
Awali, kiongozi mmoja wa waasi aliambia BBC kuwa Hezbollah imekuwa ikishambalia Syria.
Generali Selim Idriss, kwenye mahojiano na BBC alisema kuwa zaidi ya wapiganaji 7,000 wa kishia kutoka Lebanon, wanashiriki vita dhidi ya utawala wa Syria mjini Qusair, mji ambao unadhibitiwa na waasi.
Mfumo wa S-300 ni wa hali ya juu ambao unaweza kukinga makombora ya angani na ya sakafuni.
Hatua ya Urusi kuikaibidhi Syria zana kama hizo, inazua wasiwasi zaidi hasa baada ya Syria kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel, msimamo ambao pia umechukuliwa na Urusi.
Wadadisi wanasema kuwa huenda pande zinaojihusisha na mzozo wa Syria zikaanza kutumia makombora kwenye vita hivi.
Pia inahofiwa kuwa mashambulizi ya makombora yanaweza kutishia juhudi za kuandaa mkutano wa amani kuhusu Syria mjini Geneva mwezi Juni.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo sasa yamerejea katika hali nzuri ya kupambana na waasi.

Wednesday, May 22, 2013

RAIS OBAMA KUITEMBELEA TANZANIA

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ni kuwa Rais Obama anatarajia kuitembelea Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3.Na taarifa hiyo ni hii hapa:-

Monday, May 20, 2013

WATU 31 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO LA BOMU IRAQ.


Kiasi  watu  20 wameuwawa  katika  wimbi  la  mashambulio  ya mabomu  yaliyowekwa  katika  magari  katika  wilaya  inayoishi waumini  wengi  wa  madhehebu  ya  Shia  katika  mji  mkuu  wa  Iraq , Baghdad, leo.  Watu   wengine  11  wameuwawa  katika mashambulio  katika  mji  wa  kusini  wa  Basra.  Watu  kadha wameuwawa  katika  mashambulio  katika  muda  wa  wiki  moja iliyopita   wakati  hali  ya  wasi  wasi  inaongezeka   kati  ya Waislamu  wa  madhehebu  ya  Sunni  ambao  ni  wachache  nchini humo  na  Washia  waliowengi, ambao  hivi  sasa  wanashikilia madaraka  ya  serikali  ya nchi  hiyo. Idadi  ya  mashambulio imepanda  mno  tangu majeshi  ya  Marekani  kuondolewa  Desemba mwaka  2011.
Polisi  na  wafanyakazi  wa  Hospitali  wamesema  kuwa mashambulio  manane  ya  mabomu  yaliyotegwa  katika  magari katika  wilaya  ya  Washia  mjini  Baghdad , yamesababisha  vifo vya  watu  wapatao  20  leo.

Source: DW

WATU 4 WAFA NA 13 KUJERUHIWA KATIKA MSONGAMANO KANISANI.

Waumini wakiwa kanisani.
Watu wane wamekufa na 13 kujeruhiwa katika mkanyagano ndani ya kanisa la kiavengalisti nchini Ghana.
Ajali hiyo ilitokea pale waumini walipoania kufikia maji matakatifu katika tawi la kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) katika mji mkuu, Accra.
Ripoti zinasema maelfu ya watu walikuwa wamekwenda kanisani humo.
Kanisa hilo liloanzishwa na kasisi wa Nigeria, TB Joshua, ambaye anasema yeye ni mtume.
Piya amezusha utata kwa kudai kuwa anaweza kutibu magonjwa yasiyotibika kama HIV na UKIMWI.

SOURCE: BBC

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...