Monday, May 13, 2013

WANAUME 2 WATAKA WARUHUSIWE KUJINYONGA.

Huyu ni Marehemu Tony Nicklinson naye aliwahi kutaka mahakama imruhusu auawe kwa usaidizi wa daktari kwa sababu ya ulemavu wake
Wanaume wawili wenye ulemavu mbaya zaidi wanakwenda mahakamani kukata rufaa katika kesi inayoonekana kuwa moja ya kesi inayotaka mageuzi makubwa ikitaka kubadilisha sheria za serikali kuhusu haki ya mtu kufa.
Mmoja wa watu hao, Pail Lamb amekuwa na ulemavu mbaya kwa miaka mingi pamoja na kupitia uchungu mwingi, hawezi kujitoa uhai wake na anataka madaktari waruhusiwe kumuua bila ya kukabiliwa na kosa la mauaji baadaye.
Mwanamume mwingine anayejulikana kama Martin, anataka uamuzi utakaowaruhusu madaktari wamsaidie kujiua ingawa waweze kulindwa kutokana na sheria za kuweza kuwashtaki kwa kufanya kitendo cha mauaji.
Wakosoaji wanasema kuwa ikiwa mahakama itaruhusu wawili hao wajiue, itakuwa na athari kubwa kwa watu wazee na wenye ulemavu kutaka kujinyonga ili kuzuia kuwahangaisha jamaa zao kuwahudumia.

Source:BBC

KATUNI NA MECHI YA SIMBA vs YANGA MEI 18.


Friday, May 10, 2013

JOB VACANCIES - MWAUWASA

Tangazo la Kazi ya AM-MIS, AM-SO and AM-MCS

Date: 
Tuesday, May 7, 2013

MWANZA URBAN WATER AND SEWERAGE AUTHORITY     

EMPLOYMENT OPPORTUNITY


Mwanza Urban Water and Sewerage Authority (MWAUWASA) is one of the competitively best Authorities in the Tanzanian water sector supplying clean and safe water and efficient sewerage services for the residents of Mwanza City, its suburbs and other areas of jurisdiction. The Authority is hereby inviting applications from suitably qualified and experienced, dynamic and motivated Tanzanians to fill the understated vacancies that currently exist in the Authority:

Click Read more to continue.


HUU NDO WASIFU WA DAVID WILLIAM MOYES - KOCHA MPYA WA MAN UNITED.

David W.Moyes kocha mpya wa Man United.
Uongozi wa Old Trafford umetangaza rasmi na kuthibitisha kuwa David Moyes atakuwa meneja mpya wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson atakayestaafu mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Old Trafford mchana wa leo, David Moyes amepewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United kuanzia msimu ujao.
Na hii hapa chini ni wasifu wa kocha huyo mpya wa Mashetani wekundu:-

Personal information
Full name David William Moyes[1]
Date of birth 25 April 1963 (age 50)
Place of birth Bearsden, East Dunbartonshire, Scotland
Height 1.85 m (6 ft 1 in)
Playing position Centre back
Club information
Current club Everton (manager)
Youth career
1978 ÍBV Vestmannaeyjar[2]
1978–1980 Drumchapel Amateurs
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
1980–1983 Celtic 24 (0)
1983–1985 Cambridge United 79 (1)
1985–1987 Bristol City 83 (6)
1987–1990 Shrewsbury Town 96 (11)
1990–1993 Dunfermline Athletic 105 (13)
1993 Hamilton Academical 5 (0)
1993–1999 Preston North End 143 (15)
Total
535 (46)
Teams managed
1998–2002 Preston North End
2002–2013 Everton
2013– Manchester United
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.
† Appearances (Goals).

------------------
 References.

  1. ^ Hugman, Barry J., ed. (2005). The PFA Premier & Football League Players' Records 1946–2005. Queen Anne Press. p. 443. ISBN 1-85291-665-6.
  2. ^ http://www.eyjafrettir.is/frettir/2013/05/08/tyrari_ad_taka_vid_united

JOB VACANCIES - MBEYA UWSA


NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA - MUDA WA KUPOKEA MAOMBI WAONGEZWA.


Wizara ya afya imeongeza muda wa kupokea maombi ya nafasi za kazi hadi tarehe 20.05.2013 badala ya tarehe 10.05.2013.
Kwa taarifa zaidi za tangazo hilo la awali soma hapa chini.
                                           
                                           JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
                                         WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
                                                            TANGAZO LA KAZI
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa wote wenye taaluma za Kada za Afya ambao wako tayari kufanya kazi katika Utumishi wa Umma.
Vigezo na Masharti:
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Watumishi wa Kada za Afya waliojiendeleza wakiwa kazini wasitume maombi bali waombe kwa waajiri wao kubadilishwa vyeo kulingana na sifa walizopata.
4. Watumishi ambao walikwishapangiwa vituo vya kazi miaka ya nyuma na hawakuripoti au kuacha kazi hawatapangiwa vituo vya kazi, kwa sababu hawataweza kuingia kwenye ‘Payroll’ ya Serikali.
5. Maombi yote yaambatanishwe na:- Nakala ya Cheti cha Taaluma, Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita, Maelezo binafsi (CV), Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni, Nakala ya cheti cha usajili.
6. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au Wakili anayetambuliwa na Serikali.
7. Waombaji wanatakiwa kuchagua/kupendekeza maeneo matatu (Mikoa na Halmashauri) ambayo wangependa kupangiwa kazi kwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa kwenye Kibali (Tazama Tovuti ya Wizara).
2
Waajiri wote wanatakiwa kuharakisha zoezi la kuwaajiri na kuwaingiza kwenye ‘Payroll’ ya Serikali wataalam wote watakaopangiwa vituo vya kazi kwenye mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kujikimu kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima watumishi husika.
Aidha, Waajiri wanakumbushwa kukagua na kuthibitisha uhalali wa vyeti vya kidato cha Nne na Sita vya wataalam hao kabla ya kuwaajiri.
Kwa utaratibu wa mwaka huu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hatatoa barua za kupangiwa Vituo vya kazi. Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz). Ukiona jina lako kwenye Tovuti au Gazeti nenda karipoti kwenye kituo ulichopangiwa kabla ya tarehe 25 Juni, 2013 ambako taratibu za ajira yako zitakamilishwa.
Maombi yote yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Mei, 2013.
Tangazo hili pamoja na mchanganuo wa nafasi za kazi vinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz)

Wednesday, May 8, 2013

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI DR.ANTONY GERVAS MBASSA.

HOTUBA YA MHESHIMIWA DR ANTONY GERVAS MBASSA (MB) MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 (Inatolewa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge kanuni ya 99(9) toleo la mwaka 2013).


 1.0 RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA
Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuongelea au kuzungumzia hali ya sekta afya nchini bila ya kuangalia mambo makuu mawili yanayoifanya sekta hiyo kuonekana na kuiwezesha kuwa na tija. Mambo hayo makuu kwanza ni rasilimali watu katika sekta hiyo na pili madawa na vifaa vya kutolea tiba. Wizara ya afya na ustawi wa jamii ilianzisha mpango mkakati wa rasilimali watu wa mwaka 2008-2013 unaoitwa 'Human Resources Strategic Plan' unaolenga kutoa muongozo jinsi gani ya kupanga na kupambana na tatizo la rasilimali watu katika sekta ya afya lakini mpaka hivi sasa tatizo la rasilimali watu limekuwa likiongezeka kwa kasi ya ajabu na halijapatiwa ufumbuzi wa kutosha.
Mheshimiwa Spika, taarifa iliyotolewa na McKinsey & Company  mwaka 2006 kufuatia  tafiti  uliofanywa  na McKinsey & Company’s Global Public Health practice, hasa kufuatia taarifa yao waliyoito hapo mwaka 2003  inayoitwa, “ Acting Now to Overcome Tanzania’s Greatest Health Challenge: Addressing the Gap in Human Resources for HealthMapungufu ya  rasilimali watu katika sekta ya afya inaonyesha kuwa Tanzania ina upungufu mkubwa wa raislimali watu, na pia hakuna mfumo au kanuni maalum inayotumiwa na Wizara katika kugawanya  rasilimali watu chache iliyopo katika mikoa na wilaya mbali mbali hapa nchini. Jambo hili limepelekea wilaya nyingi hapa nchini kukosa kabisa  madaktari katika hospitali za wilaya.
Mheshimiwa Spika, taarifa iliyotolewa na wizara ya afya kuhusu rasilimali watu katika kada ya afya  kwa mwaka 1999 ilionyesha kuwa jumla ya watumishi wenye sifa 46,868 kwenye sekta ya afya walihitajika, lakini waliokuwepo ni  15,060 ambao ni sawa na asilimia 32.1% ya mahitaji yote, Upungufu wa watumishi 31,808 ambao ini sawa na asilimia 67.9%. Mchanganuo huo ulihusu mfumo mzima wa afya kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu ya huduma za afya.[1]
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iwaeleze watanzania toka taarifa imetolewa na Wizara na kuonyesha upungufu wa watumishi katika sekta ya afya wa asilimia 67.9% kwa mwaka 1999, sasa ni miaka 14, je ni kwa kiasi gani  imekabiliana na upungufu huo? Au taarifa zake za tafiti zinasomwa kwa wadau wa maendeleo na kuwekwa makabatini tu?

Kuendelea,Bofya Read More



MAHAKAMA KUU IMEFUTA KESI YA UGAIDI KWA LWAKATARE.

Mwandishi wa blogu hii ameripoti kutoka mahakama kuu kuwa, leo Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
 
Kwa taarifa hiyo kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
 
Taarifa zaidi zinasema kuwa ilikuwa ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
 
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

MTOTO WA MIAKA 3 AKUTWA AMEKUFA MTO MOROGORO.


Mtoto mwenye umri wa miaka 3 aitwaye Issa Iddi amekutwa amekufa katika mtkondo wa mto Morogoro eneo la Mafisa karibu na Mabwawa ya majitaka yanayomilikwa na MORUWASA.Tukio hilo limetokea leo asubuhi ambapo wakulima wa mpunga wamekuta maiti ya mtoto huyo imenasa.
Maiti ya mtoto Issa Iddi aliyekutwa amekufa mto morogoro.
Bofya Read more kuendelea.

WATU 55 WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA BOKO HARAM

Watu waliokuwa na silaha nzito jana wamekishambulia kituo cha polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na kuwauwa watu 55, ikiwa ni pamoja na polisi na raia. Msemaji wa jeshi Musa Sagir amesema shambulizi hilo lilifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu katika kituo cha polisi cha mji wa Bama, jimbo la Borno, lilisababisha vifo vya polisi 22, maafisa 14 wa gereza, wanajeshi wawili na raia wanne. Musa amesema wafuasi 13 wa kundi hilo pia walikufa katika shambulizi hilo. Kiasi ya wafuasi 200 wa kundi la Boko Haram waliokuwa na silaha nzito wanaripotiwa kuwasili wakiwa na bunduki kabla ya kuushambulia mji huo. Wapiganaji hao waliokuwa na magari aina ya pick up, kwanza waliishambulia kambi ya jeshi na kituo cha polisi kabla ya kulivamia gereza. Hakuna kundi lililotangaza rasmi kuhusika na shambulizi hilo, ijapokuwa jimbo la Borno ni ngome ya kundi la Boko Haram, ambalo maafisa wanasema ndilo lililofanya shambulizi hilo.

Source: DW

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...