Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Sunday, October 13, 2013

LEO NI LEO IGUNGA, ZITTO KABWE KUTAJA MSHARA WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Kama alivyoahidi Mbunge wa Kigoma Mashariki Mh.Zitto Zuberi Kabwe, leo anafanya mkutano na wakazi wa Wiraya ya Igunga na ameeleza kuwa miongoni wa mambo anayotarajia kuyaongelea leo ni pamoja na mshahara wa Rais na haya nai maneno yake mwenyewe:-
"Baada ya mafanikio makubwa sana katika jimbo la Nzega, leo tunaelekea Igunga. Pamoja na mambo mengine tutawaambia Watanzania ulazima wa mapato ya viongozi wa umma kuwa wazi na kutozwa kodi. Tutataja mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
Chanzo: Zitto Social media.

Friday, October 11, 2013

Kauli ya Zitto: Wabunge wa CCM wanataka kujiongezea muda wa Ubunge.Sikiliza hapa.

Speech by Dr Slaa at The University of Samford, USA .

 
Mr. President, the faculty, staff, students, invited guests and the public at large. Allow me to express my gratitude, for the cordial welcome at your lovely campus. It is one of a kind, and If I could, I would have stayed much longer to learn more on your success that I could take back to our young people. The environment and the surroundings are as beautiful as the people themselves. Along the way, I have met great people with great hearts, and I thank you for that

Likewise, receive greetings from the people of Tanzania. I was quite impressed with your level of research, and the homework you have done trying to know Tanzania, I was also particularly touched by some of you in the audience that knew the geography of my country; and even trying to challenge me . Mrs. Macquire, “People of Mto wa Mbu” are definitely
proud of you for being such a good Ambassador. We thank you, and Tanzania needs more of you that will help in exposing it to the people of America
 

Wednesday, October 9, 2013

NIA YA ZITO KABWE KUTAJA MSHAHARA WA RAIS NA MAKAMU WA RAIS, TAR. 13.10.2013 HUKO IGUNGA.

 
Mishahara ya Viongozi wa Umma lazima iwe wazi kwa umma. 
Sheria za Mishahara ziweke wazi kabisa kuwa mishahara hii itakuwa wazi na itakatwa kodi. Juzi Mpanda nimewaambia wananchi Mshahara wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa mwezi. 
Nikiwa Igunga mnamo tarehe 13 Oktoba tutawaambia wananchi mshahara wa Rais na Makamu wa Rais.
 Iwapo Rais wa marekani mshahara wake na mapato yake ni wazi na unakatwa kodi, iweje Rais wa nchi ndogo kama Tanzania. Wameifungia Mwananchi kwa kutaja viwango vya mishahara ya watumishi wa Umma. Wamfungie Mbunge kama wanaweza.
cHANZO: Zitto Kabwe Social Media.

Monday, September 30, 2013

NIA YA ZITTO KABWE JUU YA KUFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAGAZETI.

Nimetoa taarifa rasmi kwa katibu wa Bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge kwamba katika mkutano ujao wa Bunge nitawasilisha muswada binafsi wa sheria kufanya marekebisho ya sheria ya magazeti kwa lengo la kuifuta kabisa sheria hiyo.
Madhumuni ya muswada huo ni;

“kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa sababu inakizana na Katiba ya Nchi kuhusu haki za Raia kupata habari na kwamba iliorodheshwa na tume ya Nyalali ni sheria kandamizi’
...
Muswada wenyewe nitauwalisilisha siku ya ijumaa ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali uweze kuingia kwenye shughuli za Bunge zitakazoanza tarehe 15 Oktoba 2013 kwa ngazi ya kamati.

September 30, 2013
Source : Zitto social media.

Mahojiano na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Willbrod Slaa _ MAREKANI

Monday, September 9, 2013

Rais JK aonja nguvu ya CHADEMA Mwanza.

ISHARA YA VIDOLE VIWILI, PEOPLES POWER VYATAWALA
RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.
Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.
Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.
Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza.
Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!
Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio.
Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.
Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’.
Katika hatua ya kushangaza wananchi hao walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais huku wakiwazomea Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ambaye hakufika kabisa mkutanoni hapo.
Matata alionekana mapema wakati Rais Kikwete akisomewa taarifa ya maendeleo makao makuu ya wilaya hiyo lakini hakufika uwanjani kabisa katika viti vya mbele alionekana naibu wake, Swila Dede.
Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema chini kwa chini kuwa Matata ni mwizi hawataki kumsikia lakini shangwe na nderemo zikajiri pale walipotambulishwa Wenje na Kiwia.
Rais Kikwete akiwa wilaya ya Ilemela, wananchi wengi waliokuwa wamesimama njiani walimwonyesha vidole viwili ikiwa ni alama CHADEMA.
Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kumkera kiongozi huyo wa nchi pamoja na maofisa wa usalama, ambapo wana usalama wakiwemo polisi walionekana wakiwatisha na kuwazuia wananchi kunyoosha vidole viwili.
Magufuli azomewa
Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata, ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.
Adha Magufuli alizomewa pia aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM.
Pia aliendelea kuzomewa aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.
“Mheshimiwa Rais, nampongeza Meya Matata (akazomewa), lakini pia wabunge wa Ilemela na Nyamagana wanachapa kazi vizuri, nje CHADEMA lakini ndani wao CCM (akazomewa).”
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.
Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.
Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.

Friday, September 6, 2013

HIVI NDIVYO MH.MBOWE ALIVYOONDOLEWA BUNGENI JANA.

UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana misuri na askari wa bunge hilo ambapo  Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana  baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Ndugai aliwataka wabunge hao kukubaliana na matokeo yaliyotokea na kwa pamoja waweze kujadili mswaada huo 
ambao ni faida kwa taifa lakini mbali na ombi hilo kambi ya upinzani walikaidi ndipo Spika alitoa dakika tano kwa za kiongozi huyo kutoka ili bunge liendelee,ambapo hata hivyo kiongozi huyo alikaidi amri hiyo.

Baada ya mabishano hayo ndipo Spika alipotumia kiti chake na kuwataka askari wamtoe kwa nguvu nje ya ukumbi wa bunge, amri ambayo ilizua taflani na hekeheka kupelekea wabunge wa kambi ya wapinzani kuungana na kuwatunishia misuri askari hao wakimkingia kiongozi huyo kutolewa nje.

Tukio hilo lililochukua dakika zaidi ya 30 lilipelekea Bw. Job Ndugai kuwatolea macho askari hao akiwaamuru kutumia mabavu ili kuweza kumtoa nje ya ukumbi Bw. Mbowe.

Sakata hilo lilifanikiwa baada ya askari hao kutii amri ya Naibu Spika huo kwa kutumia mabavu kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzani ambapo aliungwa mkono na wabunge  kutoka nje ya ukumbi na kususia kikao hicho.

Katika tukio hilo Mwenyekiti wa vyama vyenye wabunge wengi bungeni na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjari Agustino Mrema alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wezake si cha kungwa na na kinaleta fedheha kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema yeye kutokutoka kwake nje haimaanishi kuwa ni kibaraka wa CCM na  si ndicho alichotumwa kufanya na wananchi wake,hivyo haungi mkono hata kidogo na haeleweke hivyo kuhusu msimamo wake.

"Hatoki mtu hapa nitakaa ndani ya bunge mpaka kieleweke na mnielewe kwamba mimi ndiye kiongozi wao vyama vyote tisa,hivyo nastahili kuheshimiwa na sikubaki humu ndani kwa sababu mimi ni kibaraka wa CCM bali  kinachopiganiwa ni maslahi ya taifa na ndicho nilichotumwa na wananchi wangu sikutumwa nije kutoka nje au kususia bunge."alisema Mrema.

Naye, Mbunge wa Same Mashariki na Bi Anne Kilango Malecella aliitaka Serikali kusimama imara na isiogope vitisho vinavyotolewa na wasioitakiwa mema nchi katika kupigania maslahi ya taifa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema katika kupata katiba mpya na wajumbe 156 waliopiga kura wanavigenzo vya kuweza kuchangia Mswaada huo kujadiliwa.

Vurugu za bunge hilo ziliaza toka awali katika kipindi cha muongozo wa Spika ambapo vijembe,kashifa kwa wabunge kuzungumza bila kufuata utaratibu ilimradhimu Naibu Spika Job Ndugai kusimama mara kwa mara kujaribu kurejesha utulivu katika matukio yaliyotawala Ukumbini humo. 





Mara baada ya kutolewa mwongozo ulioombwa na wabunge juzi wakidai Muswada wa Mabadiliko ya rasimu ya katiba umeingizwa vipengele kinyemele, na Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu, wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na wale wa CCM walikuwa wakituhumiana kusema uongo kuhusiana na hatua hiyo ya uandaaji wa mchakato wa Rasimu wa Katiba mpya.



Thursday, September 5, 2013

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA KUFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA SHINYANGA,MARA NA SIMIYU.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.

Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.

Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
 

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013

MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013

(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.
Muswada huu wa sasa unalenga kufanya marekebisho katika Sehemu ya Tano ya Sheria inayohusu ‘Kuitisha Bunge Maalum.’ Sambamba na mapendekezo haya, kuna mapendekezo ya kufanya marekebisho katika Sehemu ya Sita kwa kufuta vifungu vya 32 hadi 36 vya Sheria vinavyohusu utaratibu wa kura ya maoni kwa ajili ya kuhalalisha ‘Katiba Inayopendekezwa.’ Marekebisho haya yamewekwa katika aya ya 57 ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013. Mapendekezo ya Muswada huu ni muhimu lakini yana utata mkubwa.
Mheshimiwa Spika,
Katika kutekeleza majukumu yake ya kuuchambua Muswada huu, Kamati ya Bunge lako tukufu ya Katiba, Sheria na Utawala ilikutana na wadau wengi mbali mbali. Hivyo, kwa mfano, Kamati ilipata maoni ya taasisi za kidini na za kiraia; taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma; vyama vya siasa na asasi nyingine. Kwa sababu ambazo Kamati haikuelezwa vizuri na uongozi wa Bunge hili tukufu, mapendekezo ya Kamati kwenda Zanzibar kwa lengo la kukusanya maoni ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu kwa mustakbala wa Jamhuri ya Muungano yalikataliwa.
Kwa maana hiyo, ni muhimu Bunge lako tukufu lifahamu ukweli huu kwamba wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar. Kwa vile wadau wa Zanzibar walishirikishwa kikamilifu kutoa maoni yao kuhusu Muswada uliopelekea Sheria hii kutungwa mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni kwa nini uongozi wa Bunge na wa Serikali umeona si busara na sahihi kuwapatia Wazanzibari fursa ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada huu wa kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inawahusu pia Wazanzibari na nchi yao.
URAIS WA KIFALME KWA MARA NYINGINE TENA!!!!
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepigia kelele jitihada za serikali hii ya CCM kudhibiti mchakato wa Katiba Mpya kwa kuendeleza kile tulichokiita miaka miwili iliyopita, “... kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.[i] Hapo tulikuwa tunazungumzia mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wajumbe na watendaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na tulisema kwamba mamlaka hayo yalikuwa na lengo moja tu: “kuhakikisha kwamba matokeo ya kazi ya Tume hiyo ni yale tu yanayotakiwa na Rais na Serikali yake na chama chake cha CCM.
Mheshimiwa Spika,
Katika Maoni yetu wakati wa kutungwa kwa Sheria hii mwezi Novemba mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani ilipinga vikali mapendekezo ya kumwezesha Rais kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Bunge lako tukufu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Tulisema yafuatayo kuhusiana na jambo hili: “... wajumbe ... wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais.
Kwa sababu ya upinzani huo, mapendekezo ya kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiokuwa wabunge na Wawakilishi yaliondolewa katika Muswada huo wa Sheria hii. Badala yake, kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria iliyotungwa na Bunge lako tukufu kiliweka wazi kwamba “wajumbe mia moja sitini na sita [watateuliwa] kutoka ...” taasisi zilizotajwa katika kifungu hicho.
Mheshimiwa Spika,
Ni kweli kwamba kifungu cha 22(1)(c) kama kilivyotungwa kilileta giza badala ya mwanga katika suala la uteuzi wa wajumbe hao. Kama tulivyoieleza timu ya wataalamu wa Serikali kufuatia mkutano wetu na Rais Jakaya Kikwete uliofanyika Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011: “Toleo la Kiswahili la Sheria linasema kwamba wawakilishi wa makundi mengine ‘watakaoteuliwa kutoka’ kwenye makundi yaliyoorodheshwa. Toleo la Kiingereza linasema wajumbe hao watakuwa ‘drawn from’ (kwa tafsiri ya Kiswahili ‘watachukuliwa kutoka’). Maana za maneno haya hazifanani na wala hayako wazi kuhusu nani ‘atakayewateua’ au ‘kuwachukua’ wajumbe hao kutoka kwenye taasisi zao.[ii]
Kwingineko katika mkutano wetu na Rais Kikwete tulimweleza kwamba: “Wajumbe 166 wengine wanaowakilisha taasisi nje ya Wabunge na Wawakilishi hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala na taasisi zao kwani Sheria haisemi ni nani atakayewateua na/au kuwachagua.” Kwa sababu hiyo, tulipendekeza kwamba “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi.[iii]


Tuesday, August 27, 2013

TAARIFA KUHUSU KUFUKUZWA KWA MBUNGE WA KIEMBESAMAKI NA KUTEULIWA KWA MAKATIBU WAKUU WAPYA CCM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-
1.   Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.   Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.   Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013


MAKATIBU WA CCM WA WILAYA WALIOTEULIWA NA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA TAREHE 23/08/2013.

Thursday, August 22, 2013

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE LEO.

 
Kimsingi Serikali ilidanganya Bunge ili Bunge lipitishe bajeti ya Wizara ya Ujenzi mwaka 2011/12. Mawaziri Magufuli na aliyekuwa Naibu yake Mwakyembe na Waziri wa Nchi Lukuvi kwa nyakati tofauti walidanganya Bunge ili kupitisha jumla ya shilingi 252 bilioni.

PAC imeamua mawaziri hawa Waende kamati ya maadili ya bunge ili kujieleza na kuadhibiwa kwa uwongo wao.

Magufuli - 'tunaomba fedha tshs 252 bilioni kwa ajili ya KUANZA kazi za ujenzi wa barabara' - 2011...

Mwakyembe - 'fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili' 2011

Lukuvi - 'hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund' 2011

2013
CAG - 'hizi fedha za miradi hewa na kasma kivuli'.

Magufuli - ' tulilipa madeni'

Katibu Mkuu 'tulilipa madeni'

PAC ' kwanini mlidaganya Bunge'? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni? Kwanini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?

Uamuzi

CAG akague fedha zote za kasma hii hewa na kuripoti fedha hizi zimekwenda kwa wakandarasi gani na kutoa taarifa kwenye kamati mwezi oktoba.

Mawaziri wote waliodanganya Bungeni watashtakiwa kamati ya maadili na kudanganya bunge kwa lengo la kupitisha bajeti ya tshs 252 bilioni kufadhili miradi hewa.
Source:Zitto Social Media.

Monday, August 19, 2013

MTAZAMO WA ZITTO KABWE JUU YA RASIMU YA KATIBA.

Rasimu ya Katiba ibara ya 215 inasema vyanzo vya mapato ya Muungano, kikubwa, ni ushuru wa bidhaa. Wajumbe wa Tume wanasema walifanya hesabu sawa sawa na fedha hizo zitatosha kuendesha Muungano. Lazima aliyewafanyia hayo mahesabu ama aliwapotosha au hajui.
Mwaka 2012/13 Ushuru wa bidhaa (ndani na nje) uliingiza mapato ya tshs 1.5 trilioni tu. Fedha hii inatosha kuendesha Wizara ya Ulinzi peke yake!
Haitoshi hata kuhudumia Deni la Taifa (ambalo mkopaji ni Jamhuri ya Muungano). Huu muungano utaendeshwaje?
Rasimu inapaswa kufanyiwa kazi sana. Nahisi Tume ilikuwa na haraka na haikutafakari kwa kina baadhi ya masuala.
Mambo ya Muungano inabidi yaangaliwe upya kabisa ili kuboresha mfumo wa Serikali 3 unaopendekezwa ikiwemo kuzuia Washirika wa Muungano kuunda vikosi vyao vya kijeshi, Ulinzi na usalama. Suala la biashara ya kimataifa na hata suala la usimamizi wa maliasili (regulatory function).
Source:Zitto Social media.

Sunday, August 18, 2013

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE LEO.

Katika moja ya maazimio ya Kamati za Bunge za mahesabu ya Umma (Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Bajeti) iliamuriwa kuwa Serikali ianze utaratibu wa kukusanya maduhuli yake kwa kutoa risiti za kielektroniki. Azimio hilo linasema
“Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki. Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.”
Nimepitia Mpango wa Serikali wa Mapato (Volume I – Financial Statement and Revenue Estimates 2013/14) na kugundua kuwa mapato yasiyo ya kikodi yamekadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 741 kutoka Wizara, Idara na Mikoa na shi...lingi bilioni 383 kutoka kwenye Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa. Sikuweza kupata mapato ya Mashirika ya Umma maana hayaletwi kwenye Bajeti za Serikali.
Wizara 10 zinazoongoza kwa Mapato (mapato kwenye mabano ni Wizara ya Nishati na Madini ( 220 bn), Wizara ya Fedha (126bn), Wizara ya Ardhi (100 bn), Wizara ya Maliasili (84 bn), Wizara ya Mambo ya Ndani – Uhamiaji (92 bn), Wizara ya Mifugo (19 bn), Wizara ya Mambo ya Nje (16 bn) na Wizara ya Mambo ya Ndani – Polisi (17 bn), kati ya hizi shilingi 16 bilioni ni kutoka idara ya Trafiki (traffic notification fees).
Kutokana na mafanikio ya makusanyo ya VAT ambapo inaonyesha kuwa mapato ya Serikali yameongezeka kwa asilimia 60 (kutoka 500 bn mpaka 800 bn), na kutokana na rekodi mbalimbali za Serikali zinazoonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya makusanyo ya Serikali hayafiki Serikalini, ni dhahiri kuanzishwa kwa makusanyo kwa risiti za kielektroniki kutapandisha mapato ya Serikali zaidi ya mara mbili. Idara ya Usalama barabarani peke yake inasemekana kuwa makusanyo ya sasa ni theluthi tu ya makusanyo stahili kutokana na rekodi za ‘notifications’ barabarani.
Risiti za elektroniki kwa kukusanya maduhuli ya Serikali yanaweza kuongeza mapato ya Serikali maradufu na kuepuka mtindo wa Serikali wa kupandisha kodi kwenye bidhaa muhimu kwa wananchi. Uamuzi wa Kamati za Bunge za Mahesabu wa kuitaka Serikali kukusanya maduhuli yake kwa kutumia risiti za elektroniki unapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania.
 
Zitto Kabwe

MBOWE AWAKARIBISHA CHADEMA MADIWANI WALIOTIMULIWA CCM MKOANI KAGERA, AWAPA MBINU

MADIWANI wanane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Kagera waliofukuzwa uanachama wiki iliyopita wamekaribishwa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ndiye aliyewakaribisha madiwani hao wanaosubiri kufukuzwa rasmi na vikao vya Kamati Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika wiki hii mkoani Dodoma.
Madiwani waliofukuzwa na kata zao kwenye mabano ni Richard Gaspar (Miembeni), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni naibu meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uhuru wa Bukoba Mjini, Mbowe alisema CCM imewachakachua madiwani hao wanane na hata wakibaki huko chama chao hakitawaona wa maana, kwa sababu chama hicho kinalea ufisadi.
Mbowe alisema CHADEMA wako tayari kuwapokea madiwani hao waliofukuzwa na kuwafundisha siasa za mageuzi.
“Tutasimama nao katika kujenga Bukoba mpya isiyo na ufisadi kama unaofanywa na Meya wa manispaa hiyo iwapo wataamua kuja kwetu, milango ipo wazi nawakaribisha,” alisema.
Mbowe alisema CHADEMA kinamuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (CCM), anayepinga ufisadi unaofanywa na meya kutoka chama chake, Anatory Amani.
Alisema CHADEMA itashirikiana na kiongozi yeyote kutoka CCM atakayekuwa tayari kupambana na ufisadi ulioshamiri kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
“CHADEMA katika mambo ya ufisadi ina msimamno unaoeleweka na kwamba katika kupinga ufisadi kipo tayari kumuunga mkono yeyote bila kujali itikadi,” alisema Mbowe na kusisitiza kwamba hata kama meya angekuwa mwanachama wa CHADEMA kingeunga mkono afukuzwe.
“Hatuna masilahi ya kisiasa na Kagasheki lakini katika suala hili tunamuunga mkono. Nawapongeza madiwani wetu wa CHADEMA walioungana na mbunge huyo kupinga ufisadi wa meya na kusimamia masilahi ya wananchi wa Bukoba Mjini,” alisema Mbowe.
Mbowe aliikejeli CCM kuwa haiwezi kuwafukuza madiwani hao kwa sababu itakuwa imejimaliza na hawana uhakika wa kuzirejesha kata hizo ukiitishwa uchaguzi.
Alisema kutokana na hofu hiyo Makao Makuu ya CCM yaliamua kuwarejesha madiwani hao wanane waliofukuzwa na CCM Mkoa wa Kagera.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...