Thursday, September 5, 2013

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA KUFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA SHINYANGA,MARA NA SIMIYU.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.

Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.

Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
 

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...