Simba ikiwa chini ya kocha wake mkuu King Kibandeni imeonekana kuwa timu bora baada ya kuweza kusawazisha goli 3 alizokuwa ameshafungwa na mpinzani wake Yanga zilizofungwa katika kipindi cha kwanza.
Young Africans ilitoka sare ya mabao 3-3 na Simba SC katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jana katika dimba la uwanja wa Taifa
ambapo mchezo huo umeshuhudia mabao yote sita yakifungwa katika upande
wa kusini mwa uwanja.
Baada ya kosa kosa ya Hamis Kiiza dakika ya tisa ya mchezo, Mrisho
Ngassa aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 14 ya mchezo
akimaliza pasi ya Kiiza aliyewatoka walinzi wa Simba SC na Ngassa
kuukwamisha mpira wavuni.
Didier Kavumbagu alikosa bao la wazi
kufuatia mpira aliopiga kutoka seintimeta chache langoni kabla ya tik
tak ilyopigwa na Ngassa kupaa pia juu ya lango la Simba SC liliokuwa
chini ya Abeid Dhaira
Hamsi Kiiza aliipatia Young Africans bao la
pili dakika ya 35 ya mchezo, akimalizia pasi ya Mrisho Ngasa aliyemtoka
mlinzi wa Simba SC Nassoro Maoud Chollo na mpira huo kumkuta mfungaji
aliyeukwamisha wavuni.
Dakika ya 45 ya mchezo, Hamis Kiiza tena
aliipatia Young Africans bao la tatu baada ya pira uliorushwa na Mbuyu
Twite kuguswa na kichwa cha Didier Kavumbagu na kumkuta Kiiza ambaye
alifanya kazi yake ya kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 45 za
kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba SC 0 -3 Young Africans.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko, ambapo mabadiliko hayo
yaliwaongezea uhai katika dakika ya 55 uzembe wa Nadir Haroub
'Cannavaro' ulimpelekea mshambuliaji wa Betram Mombeki kuipatia timu
yake bao la kwanza.
Dakika tatu baadae kona iliyopigwa na nahodha
wa Simba Chollo ilimkuta mlinzi wa kati wa Joseph Owino akiwa peke yake
na kuukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao pili kwa wekundu wa
msimbazi.
Young Africans ilionekana kupotea kabisa kipindi cha
pili, kwani soka walilolionyesha kipindi cha kwanza halikuoneka tena
hali iliyopelekea Gilbert Kaze kuipatia timu yake bao tatu la
kusawazisha kwa kichwa kufuatit mpira wa adhabu uliopigwa na Nassoro
Masoud kumkuta mfungaji akiwa peke yake.
Mpaka dakika 90 za mchezo
zinamalizika, Simba SC 3 -3 Young Africans.
Mara baada ya mchezo
kocha mkuu wa Yanga amesema amesikitishwa na matokeo ya mchezo huo na
hasa kipindi cha pili timu yake haikucheza vizuri, na lawama akizitoa
kwa wachezaji wake kuridhika na matokeo ya kipindi cha kwanza hali
ambayo ndio iliyowagharimu kipindi cha pili.
Young
Africans: 1.Barthez, 2.Mbuyu, 3.Luhende, 4.Nadir, 5.Yondani,
6.Chuji, 7.Niyonzima, 8.Domayo, 9.Kavumbagu, 10.Ngassa, 11.Kiiza/Msuva
Subs:
Deogratia Munisi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva, Rajab Zahir,
Jerson tegete, Nizar Khalifan Simba
SC: 1.Dhaira, 2.Chollo, 3.Shamte, 4.Kaze, 5.Owino, 6.Mkude,
7.Singano, 8.Humud/Ndemla, 9.Mombeki/Pazi, 10.Tambwe,
11.Chanongo/William
Subs:
Abuu Hashim, Hassan Khatir, Issa Rashid, Zahoro Pazi, Amri Kiemba, Said
Hamisi, William Lucian
No comments:
Post a Comment