LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya
mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama
itakavyojulikana
Mara ya mwisho tuliongea ama
kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi
Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa
taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA
KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya
na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.
Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya
Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja
na mengineyo YANGA inatakiwa:
• Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza
malengo ya mradi
• Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na
mkandarasi mzuri wa mradi
• Kupata na kutenga fedha za kukamilisha
usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa upande wa BCEG
wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na
kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA
tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana
na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe
na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa
mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa
na mioundombinu ifuatayo:-
2. Hostel ya wachezaji na football academy
ya vijana
3. Viwanja vya mazoezi
4. Uwanja wa
kutosha kuegesha magari
5. Hoteli na sehemu ya makazi
6. Ukumbi
wa mikutano
7. Sehemu ya maofisi, benki, zahanati (sports
clinic)
8. Maduka, supermarket na sinema
9. Sehemu
za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)
Mara
baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City” na
kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende maeneo
ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha
mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii
itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji
miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti
mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na
kitalii.
Ili kukamilisha azma ya kuwa na
Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi ulipeleka
maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba
YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba
2012, na mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi
wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza
ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi.
Klabu ya Yanga ina
kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina
hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu
ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la
ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa
Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho
yake mahali pema peponi) na michango ya wanachama na wapenzi wa klabu
ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na haba hujaza kibaba.
Ndugu
Wandishi wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu
kuhusu michoro ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi
na BCEG limesimama, likisubiri majibu ya nyongeza la eneo. Ni matumaini
yetu zoezi hili litakamilika hivi karibuni na kuendelea na mradi.
YANGA
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
Dar es Salaam, 30
September 2013
Francis Mponjoli Kifukwe
No comments:
Post a Comment