Friday, September 13, 2013

J. MARTIN NA A.Y KUSHIRIKIANA NA VODACOM WALIPOTOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA DAR JANA.

Wanamuziki nguli Justice Martince (J.Martins) Kutoka nchini Nigeria na Ambwene Yessaya (AY) wakitoa misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Chamanzi Yatima Trust Fund kwa ushirikiano na kampuni ya Vodacom, wasanii hao walitoa wito kwa wasanii wengine kujitolea kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.

Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na watoto waishio katika mazingira magumu (Hawapo pichani) wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Chamanzi Yatima Trust Fund, walipo watembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao. Pamoja nao katika picha (waliokaa) ni wafanyakazi wa Vodacom, alie simama ni msanii Ambwene Yessaya. (AY).

Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom, (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule na Mlezi wa kituo hicho Bi. Winfrida Lubanza wakati wa utoaji wa misaada kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Chamanzi Yatima Trust Fund. Pamoja nao ni Meneja wa Chapa wa Vodacom Tanzania, Nicholous Machugu.


Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utoaji wa misaada kwa watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Chamanzi Yatima Trust Fund.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...