Thursday, September 5, 2013

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE JUU YA WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA KIGOMA.

 
Watanzania kutoka mkoa wa Kigoma waliokamatwa jana huko Tegeta wameachiwa baada ya kuingilia kati. Tumepata taarifa kuwa kuna wengine kutoka maeneo ya Kitunda pia walikamatwa jana. Tunaendelea kufuatilia. Tutaweka hapa jina la kila aliyekamatwa, kijiji anachotoka na alikamatwaje.
Tunaunga mkono juhudi zozote za kuzuia wahamiaji haramu. Hata hivyo lazima zoezi hili liendeshwe kwa umakini mkubwa sana. Nchi yetu inapakana na nchi 8. Ni dhahiri kama kila mtu anayetoka mkoa wa pembezoni ni 'suspect' wa uraia, tutagombana sana. Ni vema vitambulisho vya Taifa vitoke haraka kwa watu wa mipakani ili kuondoa hizi 'harassment'

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...