Monday, September 9, 2013

TANGAZO LA SKOLASHIPU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA SRI LANKA KWA TANZANIA KWA MWAKA 2013/2014.

Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Sri-Lanka kwa mwaka 2013/2014.

Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na fomu za maombi kwenye Kiambatisho cha tangazo hili na kuyafanyia kazi.

Maombi yaliyokamilika yakiwa na nyaraka zote zilizoorodheshwa kwenye Kiambatisho yawasilishwe Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kabla ya tarehe 15/09/2013 kwa anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...